Home Michezo UNAI AMVUA UNAHODHA XHAKA, AMKABIDHI AUBAMEYANG

UNAI AMVUA UNAHODHA XHAKA, AMKABIDHI AUBAMEYANG

0

******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kocha wa klabu ya Arsenal Unai Emery amethibitisha kuwa aliyekuwa nahodha wao Granit Xhaka hatokua na majukumu hayo tena na badala yake Aubameyang atachukua nafasi yake.

Xhaka amekua kikaangoni haswa baada ya kufarakana na mashabiki wa Arsenal na uamuzi huo utakua ni wa busara kwenye timu, maana mashabiki hawawezi kukubali timu yao iongozwe na MTU ambaye hawamkuhali tena tena mashabiki hao walifikia hadi kutishia maisha yake na ya familia yake kwa ujumla.