Home Mchanganyiko KIKAO KAZI CHA WADAU KUHUSU TATHMINI NA MAPITIO YA SERA YA MAENDELEO...

KIKAO KAZI CHA WADAU KUHUSU TATHMINI NA MAPITIO YA SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA 2000 NA MKAKATI WA UTEKELEZAJI 2005 CHAFANYIKA SINGIDA

0

 Katibu Tawala  Msaidizi Uzalishaji, Beatus Choata (katikati), akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu tathimini na mapitio ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya 2000 na mkakati wa utekelezaji 2005 kilichoanza mkoani Singida leo kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa . Kutoka kulia ni Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Emmanuel Achayo, Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Profesa Lindah  Mhando, Mkugenzi Msaidizi Sehemu ya Sera Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sophina Mjangu  na  Mratibu wa kikao hicho, Afisa  Maendeleo ya Jamii Mkuu wa wizara hiyo, Hanifa Selengu.
 Wadau wakiwa katika kikao hicho.
 Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Sera Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sophina Mjangu, akizungumza katika kikao hicho.
 Wadau wakiwa katika kikao hicho.
 Kikao kikiendelea.
 Wadau wakiwa katika kikao hicho.
 Kikao kikiendelea.
 Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Profesa Lindah  Mhando, akizungumza.
 Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Emmanuel Achayo, akizungumza.
 Mratibu wa kikao hicho, Afisa  Maendeleo ya Jamii Mkuu wa wizara hiyo, Hanifa Selengu, akizungumza.
 Washiriki wa kikao hicho kutoka Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Washiriki wa kikao hicho kutoka Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Washiriki wa kikao hicho kutoka Mkoa wa Tabora wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale,  Singida 
 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeanza kufanya kikao cha tathmini kwa kupitia upya sera ya usawa wa wanawake na jinsia ili kuangalia utekelezwaji wa sera hiyo hapa nchini ambapo kikao hicho kimeanza kwa mikoa ya kanda ya kati,  Singida, Tabora na Dodoma.
 
Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu tathmini na mapitio ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia, Katibu Tawala  Msaidizi Uzalishaji Mkoa wa Singida, Choata Beatus kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa huo,  alisema wizara iko katika mchakato wa kufanya  tathimini na mapitio ya sera ya maendeleo ya Jinsia ya mwaka 2000 na mkakati wa utekelezaji wa 2005 .
 
Beatus alisema mchakato huo unahusisha na kuwakutanisha  wadau mbalimbali katika ngazi zote ili kuwezesha kuwa na sera shirikishi inayozingatia masuala yote muhimu. 
 
“Mchakato huu utafanyika katika kanda saba, kanda hizo ni kanda ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini, Mashariki, Kanda ya Ziwa, Kusini, Magharibi na Kanda ya Kati ambapo tumeufungua rasmi leo hii “.alisema Beatus. 
 
Alisema lengo la kikao hicho ni kupata taarifa na takwimu kuhusu utekelezaji wa masuala ya usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi hususani katika sekta ya afya, elimu, kilimo, masuala ya kifedha, pamoja na uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi na siasa, mazingira, uzazi na afya ya mtoto.
 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida,  Jonathan Semiti alisema licha ya mkoa kutekeleza sera hiyo  bado kuna haja ya wadau kutoa mapendekezo pale ambapo mwanamke hajapatiwa nafasi katika jamii. 
 
 Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,  Jane Chalamila alisema mwanamke bado hajapewa nafasi ya kushiriki katika uongozi, kutoa maamuzi ngazi za kijamii hivyo kupitia kikao hicho cha wadau kitaibua masuala mbalimbali yatakayomwezesha kushirikishwa.