Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza na Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchin wakati wa mkutano wa majadiliano ya wiki ya Azaki yanayoendelea jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini waliojitokeza katika mkutano wa wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma.
Mratibu wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw.akichangia mada wa mkutano wa majadiliano ya wiki ya AZAKI inayoendelea jijini Dodoma
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKURUGENZI mtendaji wa taasisi ya Twaweza Aidan Eyakuze,amesema kuwa Asasi 16 za Kiraia (AZAKI) nchini kwa utafiti uliofanywa umesaidia kutoa mchango wa sh.Bilioni 236 kwenye uchumi wa nchi ndani ya miaka mitatu 2016 hadi 2018.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha mada ya mchango wa Asasi za kiraia kwenye uchumi wa nchi, ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma
Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kutokana na Asasi za kiraia kwa kipindi cha miaka mitatu ni sawa na kilo 2,181 za dhahabu zinazosafirishwa na kuuzwa nje ya Nchi.
“Lakini pia kiasi hicho cha fedha ambacho kimechangiwa na Asasi hizi 16, kwa kipindi hicho cha miaka mitatu ni sawa na serikali kuingiza watalii 42,316 na kukaa nchini kwa muda wa wiki moja au ni sawa lita 247 milioni za petrol,dezeli na mafuta ya taa” Amesema Eyakuze.
Pia Eyakuze amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu 2016/18 kiasi cha kodi ambazo zimelipwa na Azaki hizo 16 kwa serikali ni kiasi cha Sh. Bilioni 19.
Amefafanua kuwa kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa kwa kipindi hicho ni sawa na mapato yatokanayo na maji ya kunywa, vinywaji laini na sigara ya mwaka 2018/19 ambayo yalikuwa ni bilioni 18.8.
“Au kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa unaweza kulinganisha kabisa na kodi iliyokusanywa na Mamalaka ya maopato nchini TRA 2018/19 katika mikoa ya Rukwa, Lindi, Simiyu, Songwe na Katavi kwa pamoja ambayo makusayo yao ni Sh. Bilioni 21,” Amesema Eyakuze.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Francis Kiwanga, amesema katika wiki hiyo ya Azaki moja kati ya shuguli zitakazofanyika ni pamoja na kuwa na kongamano linalojumuisha wadau wengine ikiwemo serikali.
Amesema katika kongamano hilo wanajadiliana namna ya kushirikiana na kuweka mikakati ili mchango wa Asasi za kiraia uweze kutambulika na serikali.
Awali Mratibu wa Asasi za kiraia nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali a mitaa (Tamisemi) Denis Londo amesema Asasi la Kirai zinamchango mkubwa kwa Taifa.