Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikagua ramani wakati wa kutatua mgogoro wa Ardhi baina ya Kijiji cha Nanyala na kiwanda cha Saruji cha Mbeya, Waziri Lukuvi aliambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara kukagua eneo lenye Mgogoro kati ya Kijiji cha Nanyala Wilaya ya Mbozi na Kiwanda cha Saruji cha Mbeya.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi eneo linalotumika kuchimba madini ya Marumaru ambalo pia liko kwenye mgogoro wa Ardhi baina yao na kiwanda cha Saruji cha Mbeya, Waziri Lukuvi aliambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya(kushoto), Naibu Waziri Madini Stanlaus Nyongo na Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandege wakisikiliza maelezo kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya Kiwanda cha Saruji cha Mbeya na Kijiji cha Nanyala cha Wilaya ya Mbozi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela (aliyevaa kofia), akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutatua mgogoro wa ardhi kati ya kiwanda cha Saruji cha Mbeya na Kijiji cha Nanyala.
***********************************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza Wizara za Ardhi, Madini, Tamisemi na Viwanda zishughulikie mgogoro wa Ardhi baina ya Kijiji cha Nanyala na kiwanda cha Saruji cha Mbeya.
Mgogoro unahusisha ekari 2315 ambapo ekari 1475 zipo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na ekari 840 ziko wilaya ya Mbeya.
Leo tumekuja kama alivyoagizwa kujionea hali halisi ikiwa lengo letu ni kuumaliza mgogoro huo na tutafuata sheria taratibu na kanuni zote katika kutatua mgogoro huu.
Kufikia Jumatatu Kiwanda cha Saruji kiondoe kesi tatu zilizoko mahakamani baina ya kiwanda na wana kijiji cha Nanyala kama alivyo agiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, hii si hiyari, haiwezekani Mkuu wa Nchi anaagiza jambo halafu kuna mtu anajivuta kutekeleza.
Utoaji wa leseni za madini katika eneo lenye mgogoro usitishwe, Kijiji cha Nanyala, Wilaya za Mbozi na Mbeya zisitishe utoaji wa hati za kimila katika eneo lenye mgogoro.
Wakulima na wafugaji ambao wanalima na kufuga katika eneo hilo, mgogoro huu hauna maslahi nao hivyo wasizuiliwe kuendelea na shughuli za kilimo na ufugaji.
Wachimbaji wadogo wadogo wa chokaa wanaofanya shughuli zao kwa msimu katika eneo lenye mgogoro wasizuiliwe waendelee kufanya kazi zao.
Naibu Waziri Madini Stanslaus Nyongo
Wataalamu waangalie namna ya kubalidisha Sheria ya Service Levy ili halmashauri za Mbeya na Mbozi waweze kufaidika kwa pamoja na sio halmashauri moja kufaidika huku nyingine ikipunjwa.
Kiwanda cha Saruji cha Mbeya kama wanataka kutunza eneo kwa ajili ya matumizi ya baadaye waangalie namna bora inayotambulika kisheria na sio kukwepa gharama kwa kutofuata taratibu na sheria.
Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandenge
Halmashauri ambayo haikupata service levy na ilistahili kupata ilipwe kwakuwa tusirekebishe ya mbele bila kuangalia stahiki zilizopita za Halmashauri hizi.
Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya
Wizara ya Viwanda na Biashara ingependa kuona mgogoro huu unaisha kwakuwa kiwanda cha Saruji na vingine vilivyopo katika eneo hilo vina mchango katika maendeleo ya taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila
Migogoro inapoendelea sana lazima kuna upande unakuwa hauna uelewa hivyo wataalamu watusaidie katika hilo pia tusiingie sana katika mgogoro wa mapato kuwa yaende kwa nani isipokuwa tujielekeze kuumaliza mgogoro huo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela
Mkoa wa Songwe tunaomba kesi zifutwe ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao kwa uhuru.
Mkoa wa Songwe tunataka wawekezaji na tunawakaribisha waje kwakuwa sisi tuna mali ghafi za kutosha ila tu wajue kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe.