Home Mchanganyiko RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA BARABARA ZA MAKONGO JUU NA MADALE AMBAZO...

RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA BARABARA ZA MAKONGO JUU NA MADALE AMBAZO ZIMEKUWA ZIKILALAMIKIWA NA WANANCHI KWA UBOVU.

0

**********************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo November 01 amezindua ujenzi wa barabara za Makongo Juu na Barabara ya Madale ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikilalamikiwa kwa ubovu uliokuwa ukisababisha uharibifu wa vyombo vya usafiri, Vumbi, kupanda Gharama za usafiri na kusabbisha watu kuchelewa katika shughuli zao ambapo amewaelekeza wakandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.
RC Makonda amesema barabara ya Makongo Juu inajengwa kwa kiwango cha lami na ina urefu wa Km 4.5 ambapo ujenzi wake utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 8.9 na itachukuwa muda wa miezi 12 kukamikika ambapo ukijumuisha na gharama za fidia kwa wananchi, gharama za kuhamisha miundombinu ya umeme na maji itafikia kiasi cha shilingi Bilioni 14 ambapo amesema wananchi waliopitiwa na njia hiyo watalipwa fidia.
Akiwa kwenye Uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Barabara ya Madale yenye urefu wa Km 6 RC Makonda amesema ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.9 na mkandarasi anatakiwa kukamilisha mradi ndani ya miezi 18 kuanzia sasa.
RC Makonda amesema kukamikika kwa barabara hiyo kutawezesha watumiaji wa barabara kutumia njia ya mkato kuanzia Tegeta kutokea Wazo kuelekea Madale kutopitia Goba na hatimae kuingia Makongo na kutokea Eneo la Mlimani City jambo litakalosaidia kupunguza foleni kwenye Barabara ya Bagamoyo.
Pamoja na hayo RC Makonda ujenzi wa barabara zote hizo utajumuisha Taa za barabarani, Mitaro ya Maji ya Mvua na Sehemu ya Watembea kwa Miguu ambapo amewaomba wananchi kuwa wavumivu wakati ujenzi unaendelea.