****************************
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na Opresheni, Misako na Doria
katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kuhakikisha usalama wa raia
na mali unakuwepo ikiwa ni pamoja na wananchi kuendelea na shughuli
mbalimbali za kujitafutia kipato.
KUKAMATA SILAHA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI.
Mnamo tarehe 31.10.2019 majira ya saa 03:15 usiku huko Kijiji cha Ilaji, Kata ya
Mahongole, Tarafa Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Askari Polisi
wakiwa katika operesheni maalum walikamata silaha iliyotengenezwa kienyeji
isiyokuwa na namba inayotumia risasi za short gun nyumbani kwa mganga wa
kienyeji JOSEPH INAGA MAKUBI. Silaha hiyo ilikutwa ikiwa na risasi mbili
ndani yake. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi
kukamilika.
KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo tarehe 31.10.2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko eneo na Kata ya
Mikoroshini, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni maalum walimkamata GEORGE MWAKATUMA [26] mkazi wa mikoroshini akiwa na pombe kali aina ya WIN katoni 24 kutoka nchini Malawi bidhaa ambazo zimepigwa marufuku kuingizwa nchini.
KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo tarehe 31.10.2019 majira ya saa 13:00 mchana huko Matenki – Kasumulu, Kata ya Ikimba, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni maalum walimkamata BARIKI KYANDO [34] mkazi wa Matenki – Kasumulu akiwa na pombe kali zilizokatazwa aina ya WIN katoni 4 na chupa 32 kutoka nchini Malawi. Bidhaa hizo zimepigwa marufuku kuingizwa nchini.
KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KULIPIA USHURU.
Mnamo tarehe 31.10.2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika kizuizi cha
Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe katika barabara kuu ya Tukuyu – Kyela. Askari Polisi wakiwa katika operesheni waliwakata:-
1. FRANK MAKAYA [30]
2. SUZANA MAPUNDA [65] na
3. BALUBINA ANTHONY MSEMWA [63] wote wakazi wa Ifakara mkoani
Morogoro wakiwa na vitenge doti 55 kutoka nchi ya Malawi pamoja na unga
wa Soya pakiti 98 bidhaa ambazo hazijalipiwa ushuru. Watuhumiwa
wamekabidhiwa Mamlaka ya Mapato [TRA] Kasumulu kwa taratibu zaidi.