Home Mchanganyiko TAKWIMU ZA POLISI ZINAONESHA VITENDO VYA UKATILI WA KIJISNIA KWA WATOTO VIMEONGEZEKA...

TAKWIMU ZA POLISI ZINAONESHA VITENDO VYA UKATILI WA KIJISNIA KWA WATOTO VIMEONGEZEKA MWAKA 2018

0

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya, Mwajuma Maguiza akizungumza katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Ajenda ya wajibu wa wazazi na walezi katika malezi na matunzo ya familia inayofanyika Chuo Kikuu  kishiriki cha Dar es salaam kitivo cha Mawasiliano Kijitonyama.

………………………………………………

MIAKA 30 ya sheria ya haki za mtoto, lakini bado takwimu za jeshi la polisi hapa nchini za mwaka 2018 zinaonesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto kuongezeka kutoka matukio 13457 kwa 2017 hadi matukio 14419 kwa 2018 ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.6.

Vitendo vya ukatili ni pamoja na ulawiti, ubakaji, mimba, ndoa za utotoni, vipigo na ukeketaji vitendo hivi vyote vinagandamiza haki za mtoto zilizosainiwa na Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi ambapo zilisainiwa ili kulinda haki za mtoto.

Utekelezaji wa Sheria ya mtoto (CRC), utekelezaji wake upo lakini hautiliwi mkazo ndio maana vitendo vya ukatili vinaongezeka mwaka hadi mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya, Mwajuma Magiza, amasema kuwa kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii na familia ndio imekuwa sababu kubwa.

“Tumekuwa tukishuhudia watoto wakifanyiwa ukatili katika familia zetu, ukatili wa aina mbalimbali ikiwa wanaofanya ukatili  huo kwa kiasi kikubwa wakiwa watu waliokaribu na mtoto kama familia, dugu, jamaa na rafiki”. Amesema Mwajuma.

Hata hivyo Utafiti uliofanywa na wizara ya afya kushirikiana na wadau wa watoto kwa kipindi cha zinasema 2017 hadi Januari 2018 katika halmashauri 12 hapa nchini zinaonyesha kuwa ilibaini uwepo wa watoto 6,393 wanaofanya kazi mitaani, kati ya hao wasichana ni 1528 na wavulana 4,865.

Vilevile utafiti huo ulibaini kuwa watoto 1,385 ilibaini wanaishi na kufanya kazi mitaani usiku hii ni kutokana na kutokuwajibika kwa familia katika kumudu majukumu yao ya kuwalea watoto.

Hivyo jamii inapaswa kuwajibika katika malezi ya watoto ili kujenga taifa lenye kutengemeana kuwepo na wazazi, watoto, vijana pamoja na wazee.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya, Mwajuma Magiza akizungumza katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Ajenda ya wajibu wa wazazi na walezi katika malezi na matunzo ya familia inayofanyika Chuo Kikuu  kishiriki cha Dar es salaam kitivo cha Mawasiliano Kijitonyama kutoka kushoto ni Francis Othiambo Kaimu Mwakilishi mkazi wa UNICEF Tanzania na katikati ni Tausi Mwilima Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sehemu ya Familia na Elimu ya Malezi.

Francis Othiambo Kaimu Mwakilishi mkazi wa UNICEF Tanzania akisoma hotuba yake katika semina hiyo kulia ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya, Mwajuma Magiza na katikati ni Tausi Mwilima Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sehemu ya Familia na Elimu ya Malezi

Tausi Mwilima Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sehemu ya Familia na Elimu ya Malezi akizungumza katika semina hiyo.

Picha mbalimbali zikionesha washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam mbalimbali wa masuala ya haki za watoto.