Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi ( AG) akifungua Mkutano baina yake na wakati akifungua mkutano baina yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.Mkutano huu wa siku mbili unafanyia Jijini Dododma.
Sehemu ya Wajumbe wanaohudhuria Mkuwano wa Siku mbili ambao umeitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Washiriki wa Mkutano huu ni Mawakili wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi za Serikali, Mashirika na Halmashauri za Miji.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo kwa
Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba, zinawasilisha
taarifa zote zinazohusu mashauri ya madai zinazohusiana na
taasisi hizo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi,
ameyasema hayo leo jumatano, wakati akifungua mkutano baina
yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za
Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka za Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi
mbalimbali za Serikali.
Zaidi wa wajumbe 300 kutoka taasisi hizo wamehudhuria Mkutano
huu ambao ni wa siku mbili, unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma,akiwamo pia Wakili Mkuu wa
Serikali, Dkt.Clement Mashimba (SG).
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,taarifa hizo
zinatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Profesa Kilangi, amewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba,
Ofisi yake imeamua kutoa maelekezo hayo kutokana na kuwepo kwa
changamoto ya baadhi ya taasisi za serikali kuendesha kesi
zake bila taarifa ya uwepo wa kesi hizo kuwasilishwa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa
Serikali.
Changa moto hii ya baadhi ya Taasisi kuendesha kesi zake pasipo
kutoa taarifa kwa Ofisi hizo mbili kumeisababishia serikali
hasara ambayo ingeweza kuzuilika.
“Ipo changamoto ya baadhi ya taasisi za serikali kuendesha kesi
zake bila taarifa kuwasilishwa Ofisi ya yangu na ofisi ya Wakili
Mkuu wa Serikali, ,utaratibu huu umeisababishia hasara
serikali hasara ambayo inegeweza kuzuilika”.
“Hivyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo
kwa taasisi zote za serikali kuwasilisha taarifa zote za mashauri ya madai kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali Mkuu wa Serikali kwa hatua zake
stahiki”.Amesisitiza AG.
Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema,
Ofisi yake pia ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa
mfumo maalum wa kieletroniki wa uwasilishaji wa taarifa kwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka katika Taasisi mbalimbali
baina ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara na
Taasisi zake.
Vile vile Profesa Kilangi ameeleza kwamba, Ofisi yake imesajili
Jarida litakalochapisha masuala Muhimu ya sheria yanayohusu
Mihimili ya Dola ( The Journal of Government Law). Lengo la
jarida hilo litakuwa ni kutoa fursa kwa mawakili wa Serikali
kuchapisha makala mbalimbali zinazohusu mihimili ya Dola.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Kilangi ameitisha Mkutano
huu kwa madhumuni kadhaa yakiwamo ya kuiwezesha Ofisi yake
kujadiliana na kubadilishana mawazo na Wajumbe kutoka Taasisi
hizo juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na uoaji wa huduma
za kisheria hapa nchini.
“Kama mnavyofahamu jukumu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni
kutoa ushauri katika masuala yote ya kisheria jukumu ambalo pia
nyinyi mnalifanya kwa katika maeneo yenu kwa niaba ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hivyo kikao hiki ni muhimu sana
kwetu sote ili tupeane taarifa na miongozo mbalimbali
inayohusiana na utekelezaji wa majukumu hayo kwa lego la
kuongeza tija na ufanisi wa kazi”. Akasema Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Kuhusu kuanzishwa kwa Daftari la Mawakili, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali amesema, Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Kifungu cha 16A kama
ilivyorekebishwa, inampa mamlaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuanzisha Daftari la Mawakili wote walioko kaitka Utumishi wa
Umma nchini ( Rolle of State Attorneys).
Akasema, Daftari hilo, litakuwa lina taarifa mbalimbali za
Mawakilil hao na pia litasaidia sana kufahamu wakili gani yupo
wapi na ana taaluma gani au amebobea katika fani gani ili hatimaye pale serikali inapomhitaji kwa jambo fulani aweze kupatikana kwa urahisi.
Aidha kupitia Dafteri hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ataweza kutambua mahitaji ya aina ya mafunzo kwa ajili ya
kuongeza uwezo na ubobezi wa mawakili wa Serikali katika maeneo
mbalimbali.
Mada mbalimbali zikiwalishwa katika siku hii ya kwanza ya
mkutano zikiwamo zinazohudu vazi maalum ( joho) litakalovaliwa
na Wanasheria wa Serikali wanapokwenda Mahakamani au katika
shughuli maalum za kitaaluma.
Lengo la kuwa na Joho maaluma kwa Mawakili wa Serikali
wanaokwenda Mahakamani pia litawezesha kutambuliwa kirahisi kwa
Mawakili wa Serikali, pia litawaongezea kujiamini, kuaminika na
kukubalika.