Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

0

JESHI LA POLISI MKOA WA  MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA VIKIWEMO VILE VYA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA  VILIMKAMATA RAIA MMOJA WA INDIA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MADINI AINA YA ALMASI BILA KIBALI NA KINYUME CHA SHERIA. UFUATILIAJI WA UKAMATAJI ULIANZA TAREHE 23/10/2019 MAJIRA YA 11;00 HRS  ENEO LA UWANJA WA NDEGE JIJINI MWANZA. RAIA HUYO WA INDIA YOGESH SUMATLAL SHAH MIAKA 44, MWENYE HATI YA KUSAFIRIA NAMBA R9800410 ALIKUWA KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUSAFIRI KUTOKA MWANZA KUELEKEA NAIROBI KENYA KWA KUTUMIA NDEGE YA PRECISION NA ALIKAMATWA KATIKA ENEO LA UPEKUZI AKIWA NA MADINI YA ALMASI YENYE UZITO WA GRAMS 50 YENYE THAMANI YA USD 282,898.07 SAWA NA TSHS 650,980,853.34/= ALIKUWA AMEFICHA MADINI HAYO NDANI YA MKONO WA BEGI LAKE. UPELELEZI   KUHUSIANA NA TUKIO HILI KWA HATUA YA AWALI UMEKAMILIKA NA MTUHUMIWA LEO ANAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA MATATU AMBAYO NI,

1) KUSAFIRISHA MADINI BILA KIBALI

2) KUFANYA MAKOSA YA KIMTANDAO NA

3) KUTAKATISHA FEDHA

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA ILI KUBANA NA KUZIBA MIANYA YOTE INAYOTUMIWA NA WAHALIFU KUIBA RASILIMALI ZA TAIFA HILI NA KILA ATAKAYEKAMATWA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA . AIDHA WANANCHI WANAHAKIKISHIWA KUWA KIPINDI CHOTE CHAMCHAKATO  WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA UTAKAO FANYIKA TAREHE 24 MWEZI NOVEMBA MWAKA HUU USALAMA KWA VYAMA VYOTE NA WANANCHI KWA UJUMLA UMEIMARISHWA. WATU WAJITOKEZE KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOWALETEA MAENDELEO.         

 IMETOLEWA NA;

Muliro J. MULIRO- ACP

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

31OCTOBER,2019.