Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameridhishwa na hali ya amani na usalama inavyoendelea wakati wa zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa kugombea nafasi mbalimbali uchaguzi Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji 2019.
Gavana Shilatu amejionea hayo alipotembelea maeneo mbalimbali ndani ya Tarafa ya Mihambwe na kujionea namna utaratibu unaendelea wa wagombea wanachukua fomu na hali ilivyo mitaani na kutoa rai ya amani na usalama izidi kuimarishwa.
“Nimepita kujionea utaratibu unavyoendelea wakati wa zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea na Wafuasi wao. Nazidi kusisitiza demokrasia iendelee kuwa chachu ya kudumisha amani na usalama uliyopo.” Alisema Gavana Shilatu.
Uchaguzi Serikali za mitaa vijiji na vitongoji 2019 unashika kasi ambapo upo kwenye hatua ya kuchukua na kurudisha fomu lililoanza Oktoba 29 hadi Novemba 4, 2019.