Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akisitiza jambo kwa mkandarasi GS Eng & Const. na wasimamizi wanaojenga daraja jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na barabara unganishi KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akimwelekeza jambo mmoja wa wasimamizi wanaosimamia ujenzi wa daraja Jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi daraja Jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na barabara unganishi kilimota tano KM 5.2 ikiendelea jijini Dar es Saam.
Kazi ya ujenzi wa daraja Jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na barabara unganishi kilimota tano KM 5.2 ikiendelea jijini Dar es Salaam.
***************************
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa ameelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo leo, amempongeza mkandarasi GS Eng & Const. kutoka Korea Kusini na wasimamizi wanaojenga daraja hilo kwa kasi inayoendana na makubaliano ya mkataba.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri inayoendelea katika ujenzi wa mradi huu na nawaagiza wataalam wote wa wizara wanaoshiriki katika mradi kujifunza kikamilifu ili tupate hazina ya wataalam wengi zaidi,” amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo, Eng. Lee Suk Joo amesema wamejipanga kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na pia kuongeza idadi ya wataalamu wa madaraja haoa nchini.
Daraja jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na upana wa mita 20.5 litakalo kuwa na njia nne za magari, njia za watembea kwa miguu pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 linataraajiwa kukamilika mwaka 2021 na kupunguza kiasi kikubwa msongamano wa magari katikati
ya jijini la Dar es Salaam.