Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni, Ndugu Aron Kagurumjuli aliyesimama,
akisisitiza jambo kwa madiwani waliokuwa kwenye kikao
maalumu cha robo ya mwaka katikati ni Mstahiki Meya
Benjamini Sita, na kushoto ni Naibu Meya George
Manyama.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni , Ndugu Aron Kagurumjuli akisoma taarifa ya
utendaji kazi na uwajibikaji wa idara na vitengo
mbalimbali pamoja na tathimini ya bajeti ya mwaka
2018/2019.
Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wakijadiliana
mambo mbalimbali.
***********************************
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni limemchagua Mhe.George Manyama kutoka
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Meya wa
Halmashauri hiyo kwa awamu ya nne tangu mwaka 2016.
Uchaguzi huo umefanyika leo (jana) katika baraza
maalumu la madiwani la robo ya mwaka ambapo jumla
ya wajumbe 21 ambao ni madiwani walishiriki uchaguzi
huo.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu tawala wa Halmashauri
hiyo Bi Stella Msofe amesema kuwa idadi ya kura
zilizopigwa ni 21 kulingana na wajumbe wa baraza hilo
kutoka vyama vyote vyenye madiwani katika baraza hilo.
Msofe amemtangaza Mhe. Manyama kutoka CCM kuwa
mshindi wa nafasi hiyo ya Naibu Meya kwa kupata kura
13, huku mpinzani wake Mhe. Phares Lupomo kutoka
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akipata
kura nane.
Awali wagombea hao wawili walipata nafasi ya kunadi
sera zao kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo ikiwa ni
utaratibu wa kawaida kwa wagombea wanafasi
mbalimbali.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Aron
Kagurumjuli alimuapisha Diwani mteule mpya wa viti
maalumu Mhe. Caroline Kazinze aliyekuwa chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema kabla ya kujiunga
na CCM.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya
kuapishwa , Caroline amesema kuwa anamshukuru
nakumpongeza Rais Dk, John Magufuli kwa kazi nzuri
anayoifanya yakuwaletea wananchi maendeleo.
Amefafanua kuwa kuondoka kwake Chadema
kunatokana na kazi nzuri anayoifanya na kwamba hakuna
kitu cha kupinga zaidi ya kumpongeza,kama maendeleo
tunayaona anafanya kwa vitendo.
Amesema kuwa “ sina sababu ya kuendelea kupinga
maendeleo ambayo anafanya Rais wetu Dk. Magufuli ya
kutetea wanyonge, wakina mama wajane, mimi ni mama
amenigusa kwenye utendaji wake wakujali wakina
mama.
Aidha Mhe. Caroline amesema “ CCM imenishawishi
,inafanya kazi kwa vitendo, rais anapita kila kijiji kusikiliza
kero za wananchi nakuzitatua, CCM imekuwa mpya
,upinzani sikuhizi hawana cha kupinga ,ninawashauri
wote tumuunge mkono Rais wetu.
Hata hivyo baraza hilo pia limepitisha kwa pamoja
taarifa ya utendaji kazi na uwajibikaji wa idara na vitengo
mbalimbali pamoja na tathimini ya bajeti ya mwaka
2018/2019 sambamba na kupanga kamati mbalimbali za
halmashauri hiyo.