*************************************
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amevunja bodi ya kiwanda cha maziwa Njombe na kumfuta kazi meneja wa kiwanda hicho Edwin Kidehule kwa madai ya kushindwa kusimamia ipasavyo na kusababisha kiwanda hicho kudaiwa fedha nyingi na wafugaji wa ngo’mbe za mauzo ya maziwa.
Mbali na madeni kiwanda cha maziwa Njombe ambacho kinamilikiwa kwa mfumo wa hisa na chama cha wafugaji NJORIFA,Kanisa la cathoric,Halmashauri ya mji pamoja na halmashauri ya wilaya ya Njombe pia kimetajwa kupata hasara ya mil 12 Octoba mwaka huu ya mauzo ya maziwa mashuleni jambo ambalo limeikasirisha serikali na kulazimika kuvunja uongozi mzima wa kiwanda hicho.
Akitoa maagizo ili kunusuru kiwanda hicho katika mkutano wa dharura uliokutanisha wamiliki mkuu huyo wa wilaya ameagiza kusimamishwa kazi mara moja meneja wa kiwanda kuwa kushindwa kusimamia ipasavyo kiwanda hicho na kusababisha hasara,kutolipa madeni ya mauzo ya maziwa kwa wafugaji,kuwanyonya wafugaji wa Njombe kwa kununua maziwa kwa sh 600 ili hali maziwa yanayonunuliwa nje ya mkoa huo yakinunuliwa kwa shilingi 1200.
Ametaja sababu nyingine kuwa ni lugha chafu,kutoa taarifa za uongo kwa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya kuhusu ununuzi wa maziwa wilayani Mbalali huku nyingine zikiwa ni utoaji wa ajira kwa watu wasio na sifa kwa kujuana jambo ambalo linamewafanya wafugaji wengi ambao licha ya kuwa na umiliki katika kiwanda hicho kugoma kuendelea kuuza maziwa kiwandani hapo.
Uamuzi wa mkuu wa wilaya wa kuivunja bodi ya kiwanda ambao umekwenda sambamba na kumfuta kazi meneja pamoja kuwataka wafanyakazi wote katika vitengo muhimu kusimamishwa kazi na kutakiwa kutuma CV zao ili kuomba kazi upya kwa lengo la kuondoa kabisa mizzi ya wizi na uhujumu ambayo ilipandikizwa kiwandani hapo inapokelewa kwa mikono miwili na wafugaji ambao wanadai walipoteza kabisa imani na uongozi, kama ambavyo wanaeleza wafugaji akiwemo Edward Mpete,
Suala lingine ambalo limeifanya serikali kuchukua hatua ili kunusuru kiwanda hicho ni hasara ya mil 12 ambazo kiwanda hulipwa baada ya kusambaza maziwa mashuleni kama ambavyo meneja wa mradi wa EADD kupitia shirika la HEIFER International kanda ya nyanda za juu kusini anavyoeleza.
Kiwanda cha maziwa Njombe kina uwezo wa kupokea zaidi ya lita elfu 20 kwa siku lakini inadaiwa uongozi mbovu usiona na ubunifu umesbabisha wafugaji wengi kuuza mitaani maziwa na wengine kuuza mikoa jirani na kusababisha kiwanda hicho kupokea lita elfu 3 kutoka elfu 20 kwa siku.