Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB – Donatus Richard (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mohamed Mussa ambaye ni NMB Wakala katika Mtaa wa Livingstone, Kariakoo.
MKUU wa Masoko wa Benki ya NMB – Rahma Mwapachu (wapili kushoto) akimhudumia mteja wa benki – Petra Karamagi katika Tawi la Oyster Plaza.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB – Omari Mtiga (katikati) akimsaidia mteja kujaza fomu ya kuweka fedha katika Tawi la Zanzibar.
Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali NMB – Vicky Bishubo, akizungumza na mteja wa benki hiyo – Nyamate Mayunga, alipomtembelea dukani kwake.Kushoto ni Meneja wa Tawi la Gongo la Mboto – Rehema Mwibura.
************************************
Benki ya NMB imeendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja kwa kuwafikia kwa ukaribu zaidi wateja wao.
Viongozi Waandamizi wa benki hiyo wameingia kwenye matawi mbalimbali yaliyopo kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar kuwahudumia wateja waliofika kupata huduma.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar – Idd Badru amesema programu hiyo waliyoiita ‘Make A Difference’ imelenga kuwaweka karibu watendaji wa benki na wateja wao wa kada zote.
Amesema kupitia njia hiyo wameweza kukutana na wateja wao na kujua kitu gani wanahitaji ili kuendelea kuboresha huduma wanazozitoa.
“Imekuwa ni siku nzuri kwanza wateja wamefurahi, wamekutana na viongozi wetu Waandamizi na wamewahudumia katika matawi yao na kuwatembelea katika maeneo yao ya biashara ”
“Pili imetupa fursa ya kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo na imekuwa rahisi pia kuzipatia ufumbuzi kwa kuwa wengine wamekutana na wafanya maamuzi. Mengine yamechukuliwa yataenda kufanyiwa kazi kupata ,” amesema Badru
Akizungumzia hilo mfanyabiashara wa Tandika Gamsa Moniko amesema hatua hiyo imewapa furaha wateja na kujiona wa thamani kwa benki ya NMB
“Mimi ni mteja wa kawaida Ila kwenye biashara yangu nilitembelewa na Meneja wa tawi pamoja na watu kutoka Makao Makuu, binafsi ilinipa faraja kwamba wamenitambua na kuona mchango wangu kiasi cha kunitembelea,” amesema Moniko
Naye Richard Njau ambaye ni Wakala wa NMB ameeleza kuwa kupitia programu hii ameweza kuwasilisha changamoto zake moja kwa moja kwa watendaji wa benki.
Kwa upande wake Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo Abella Tarimo amesema kitengo chake kitaendelea kuyafanyia kazi maoni ya wateja ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka changamoto zilizoainishwa kwa kuwahakikishia wateja kuwa Ubora Upo NMB.
#NMBKaribuYako