NJOMBE
Kwa mara ya Kwanza serikali mkoani Njombe kwa kushirikiana wadau imeanzisha maonesho ya siku tatu ya kilimo,ufugaji na uvuvi kwa lengo la kusogeza fursa kwa wananchi kujifunza kwa vitendo pamoja na kutanua wigo wa masoko ya bidhaa na malighafi wanazozalisha mkaoni humo.
Afungua maonesho hayo ya mkoa wa Njombe mgeni rasmi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri pamoja na mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge wamewataka wakulima, wafugaji na wavuvi mkoani humo kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu kwa vitendo juu ya matumizi zahihi ya pembejeo na dawa za kutibu mifgo .
Katika hatua nyngine viongozi hao wa serikali wamezitaka taasisi zinazohusisha na usimamizi wa biashara ikiwemo TAN TRADE na zinazohusika na upimaji wa udongo kuhakikisha zinashiriki maonesho hayo ambayo ni muhimu zaidi katika mkoa wa Njombe amekuwa kinara katika uzalishaji wa mazao ya chakula ili kutoa elimu na ushauri kwa wananchi.
Mara baada ya uzinduzi wa maonesho ya kilimo ,uvuvi na mifugo kuzinduliwa suala la mwamko wa wananchi kujitokeza katika viwanja vya maonesho limeonekana kuwa tatizo jambo ambalo linamsukuma mkurugenzi wa kampuni kongwe ya kilimo na ufugaji ya Mpete General Traders Erasto Mpete kuwataka wana Njombe kujitokeza ili kupata elimu kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa serikali, mashirika na taasisi juu ya matumizi bora ardhi na pembejeo.
Kuhusu kuitumia fursa hiyo Mpete amesema wazo la maonesho limefanyika katika muda muafaka wa maandalizi ya mashamba kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo hivyo jamii ihamasike kushiriki ili kunufaika na elimu na kupata soko la mazao yanayozlishwa.
“Maonesho haya yanapaswa kuendelezwa kwasababu yanafaida kubwa kwa wakulima na wananchi kwa ujumla , kufahamiana na kutanua wigo wa biashara hivyo naomba wananchi tujitokeze kuona bidhaa na huduma zinazotolewa katika maonesho haya” alisema Erasto Mpete.
Nae bwana shamba wa mkoa wa Ruvuma na Njombe kutoka kampuni ya YARA akielezea maandalizi yaliofanywa na kampuni hiyo kwa ajili kutoa huduma bora amesema kampuni imetoa mafunzo kwa wakulima vijijini pamoja na mawakala wao ili kumpa huduma stahiki mkulima na kwamba jitihada za kuendelea kusogeza huduma jirani kwa wakulima zinaendelea.
Aidha Mwangomile ametoa hofu wakulima juu ya upatikanaji wa pembejeo kwa madai ya kwamba kampuni ina hazina ya kutosha ya mbolea hivyo wakulima wanapaswa kuendelea na maandalizi ya mashamba bila hofu yeyote na kueleza hisia zake kuhusu kuanzishwa na maonesho ya kilimo katika ngazi ya mkoa.
“Kiujumla tunashukuru sana waasisi wa maonesho haya katika ngazi ya mkoa kwasababu yanatoa fursa kwa wakulima,wavuvi na wafugaji kukutana na watalaamu na kuhoji juu ya yanayowatatiza”alisema bwana shamba wa YARA Mwangomile.
Katika mambo mengine ambayo yamezungumzwa na washiriki ikiwemo kampuni ya Mtewele General Traders ndugu Roden Ulanga ambaye ni bwana shamba wa kampuni anasema amefurahishwa na fursa ya maonesho kwa kuwa makampuni yanatangaza huduma zake .
Akitoa rai kwa wakulima bwana shamba huyo amewataka wakulima kuachana na kilimo cha mazoea na badala yake wafate ushauri wa kitaalamu katika matumizi ya mbolea na viuatilifu vingine ili waweze kupata tija katika shughuli za kilimo.
Pia Ulanga ameshauri wakulima kuanza kupima udongo wa mashamba yao ili kuweza kujua kiwango cha rutuba na aina ya mbolea inayopaswa kutumika hatua ambayo itawafanya kupata mazao bora na yenye ushindani sokoni.
Katika maonesho haya kampuni ya kimataifa ya Olivado kutoka nchini Newsland imetuma mwakilishi wake Bosco Richard ambaye ni meneja wa kiwanda kilichopo Itulahumba wilayani Wangi’ombe kuonyesha bidhaa yake ya Mafuta ya chakula yanayokamuliwa kutoka kwenye tunda la parachichi ambalo linazalishwa kwa wingi mkoani Njombe ambaye anawataka wakulima kuwekeza katika kilimo hicho ili kupata chenye tija kubwa sokoni.
Meneja huyo amesema kuna kila sababu ya wakazi wa njombe kuchangamkia kilimo hicho kwa kua zao la parachichi linatumika kuzalisha bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta ya chakula na kupaka mwilini na kudai kwamba hata tunda lililo oza linasoko duniani.
Maonesho Hayo Yenye Kauli Mbiu ya ”Zalisha Mazao ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kwa Tija ,Tanzania ya Viwanda”yafanyika kwa siku tatu kuanzia octoba 25 hadi 27 huku yakihudhuliwa na makampuni na taasisi mbalimbali ,wadau wa kilimo,wananchi na viongozi wa serikali.