Mwanachuo kutoka Nyanda za Juu Kusini Gwantwa Thomson akishiriki mashindano ya kuruka chini wakati wa Mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu yanayoendelea Mkoani Mtwara
Mwanachuo Salama Mohamed kutoka Kanda Magharibu akishiriki mashindano ya Kuruka chini wakati wa mashindano ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu yanayoendelea Mkoani Mtwara. Mashindano yanafanyikia katika viwanja wa Chuo cha Ualimu Mtwara Kawaida
Mwanachuo Janet Jacob kutoka Kanda ya Kati akishiriki mchezo wa kuruka chini katika Mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu yanayoendelea Mkoani Mtwara
………………
MASHINDANO ya kitaifa ya michezo na sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania bara(UMISAVUTA),yameendelea kushika kasi mkoani Mtwara
Baadhi ya wanachuo kutoka kanda mbalimbali wakishiriki mchezo wa kuruka chini katika viwanja vya chuo cha Ualimu Mtwara Kawaida wakati wa mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara yanayoendelea Mkoani Mtwara
Mashindano hayo yalianza jana na oktoba 25 na yatafikia tamati Oktoba 31, mwaka huu huku yakiwa yanajumuisha zaidi ya washiriki 5,600 kutoka vyuo vya ualimu vya serikali 35.
Kesho ndo utakuwa ufunguzi rasmi utafanyika katika uwanja wa Nagwanda Sijaona na mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye atakuwa anamwakilisha Waziri Mkuu.