*****************************
Na Mwandishi wetu Arusha
Makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu anatarajiwa kufungua semina kwa ajili ya wabunge wanawake kutoka nchi zaidi ya kumi barani Afrika ambao ni wanachama wa chama cha wabunge wanawake jumuiya madola
Akiongea na vyombo vya habari mkoani Arusha Katibu Msaidizi wa Ukanda wa Afrika bw Jakubu Saidi alisema kuwa semina hiyo inalenga kuboresha na kuongeza idadi kubwa ndani ya mabunge
Alifafanua kuwa wana semina hao wataweza kujadili na kupata elimu mbalimbali kutoka kwa wanawake ambao waliokuwa kwenye mabunge au tasnia mbalimbali kwa ajili ya kujifunza zaidi
“kwa Tanzania tuna mama anna makinda huyu alikuwa Spika wa bunge ana mengi ya kuwafundisha lakini pia tuna mheshimiwa Mboni mhita huyu ni mbunge mpya ndani ya bunge wote hawa pamoja na wengine wataweza kupata semina ambayo itabebwa na mada kama 5 “aliongeza
Pia alisema Kuwa kwa nchi za madola Afrika nchi ya Rwanda ndio nchi yenye wabunge wengi ambapo bunge zima lina asilimia 61huku kwa tanzania ikiwa ni asilimia 36.
Alihitimisha kwa kusema wabunge hao siku ya jumatatu watatembelea katika vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika mkoa Wa arusha kwa ajili ya kujionea mazuri na vivutio vya tanzania
Semina hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na spika wa bunge la jamuhuri wa muungano wa tanzania