Home Mchanganyiko WAMILIKI WA MAROLI WAMETAKIWA KUTAMBUA MAJUKUMU YA TAMSTOA

WAMILIKI WA MAROLI WAMETAKIWA KUTAMBUA MAJUKUMU YA TAMSTOA

0

*********************

NA EMMANUEL MBATILO

Wamiliki wa Malori Makubwa yanayobeba mizigo wametakiwa kufuatilia ni namna gani chama cha Wamiliki wadogo na Wakati wa Maroli wanavyofanya kazi ili kuweza kutambua majukumu yao.

Ameyasema hayo leo Mwenyekiti wa Wamiliki wadogo na Wakati wa Maroli Tanzania(TAMSTOA) Bw.Chuki Shabani katika ofisi za Chama hicho.

Akizungumza na Wanahabari Bw.Chuki amesema kuwa Wamiliki wengi wa maroli wanatumia watu wa kati kufuatilia masuala ya chama hivyo wengi wao wanashindwa kupata taarifa kamili kotoka kwenye chama.

“Tunaomba mwaka huu wamiliki wa maroli wote wanahakikisha taarifa kamili za kufikika kwao taarifa za nini chama wanafanya”.Amesema Bw.Chuki.

Aidha, Bw.Chuki amesema kuwa wanachama wengi wameshindwa kukitumia chama chao ipasavyo kutatua matatizo yao kwasababu hawana anuani kamili ya chama na viongozi wa Chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha madalali wa maroli ya kusafirisha mizigo mikubwa Tanzania Bw.Rajabu Masasi amesema kuwa usajili wa chama hicho haujakamilika hivyo amewataka ofisi ya usajili kuharakisha usajili kufanyika ili waweze kuchangia pato la taifa.

“Lengo la chama hiki ni kujaribu kuwaweka wafanyabiashara wanaowapatia kazi kuwa sehemu salama ili kuweza kuondokana na udanganyifu ambao wamekuwa wakijitokeza”. Amesema Bw.Masasi.