Home Biashara TanTrade yawataka wadau wa sekta ya Maonesho kuzingatia sheria na kanuni

TanTrade yawataka wadau wa sekta ya Maonesho kuzingatia sheria na kanuni

0

Mkurugenzi Mkuu akifungua mkutano wa wadau kwaajili ya kukusanya Maoni
yenye lengo la kuboresha kanuni za sheria TanTrade ya udhibiti wa Maonesho
ndani na nje ya nchi uliofanyika tarehe 24 Oktoba, 2019 katika ukumbi wa
mkutano wa Arnautoglu, Jijini Dar es SalaamWaandaaji wa Maonesho na Misafara ya Kibiashara Ndani na Nje ya Nchi,
Wamiliki wa Kumbi za Maonesho, Wajenzi wa Vizimba vya Maonesho, Wizara,
Taasisi za Umma na Binafsi wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa sheria za
TanTrade kwenye mkutano ulioandaliwa na TanTrade kwa lengo la kukusanya
Maoni yenye lengo la kuboresha kanuni za sheria TanTrade ya udhibiti wa
Maonesho ndani na nje ya nchi uliofanyika tarehe 24 Oktoba, 2019 katika
ukumbi wa mkutano wa Arnautoglu, Jijini Dar es Salaam.

*************************************

Waandaaji wa Maonesho na Misafara ya Kibiashara Ndani na Nje ya Nchi, Wamiliki wa Kumbi za Maonesho, Wajenzi wa Vizimba vya Maonesho, Wizara, Taasisi za Umma na Binafsi zinazohusika na maswala ya biashara pamoja na wadau wote kwa ujumla wanatakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uandaaji wa Maonesho ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) alipokuwa akifungua mkutano wa wadau ili kutoa maoni ya kanuni mpya za sheria ya TanTrade uliofanyika tarehe 24 Oktoba, 2019 katika ukumbi wa Arnautoglu, Jijini Dar es Salaam.

“Hakuna asiyejua kumekuwa na utitili wa Maonesho na tumebaini baadhi ya waandaaji hawalengi kuendeleza bidhaa na kuwawezesha wafanyabiashara kuonesha walichonacho ili wapate wanunuzi na masoko endelevu, kama Taasisi yenye Mamlaka haiwezi kunyamaza tunawajibu wa kumlinda mfanyabishara anayetafuta masoko” amesema Bw Rutageruka.

Ameendelea kusema baadhi ya waandaaji wa Maonesho hutumia kumbi ambazo
hazizingatii viwango na masharti ya kumbi za Maonesho ili kulinda usalama wa
washiriki na watembeleaji wa Maonesho kama vile kumbi kuwa na milango ya dharula, vifaa vya zimamoto na eneo la kukusanyikia wakati wa dharula.

Ameongeza kwa kusema kuwa baadhi ya waandaaji hawazingatii usalama wa kumlinda mtumiaji wa bidhaa zinazooneshwa kwenye Maonesho hayo na baadhi ya waandaaji hawazingatii aina ya bidhaa zinazotakiwa kuoneshwa maana mwelekeo wa muandaaji ni kujipatia kipato tu.

Naye Bw. Deogratius Kilawe kutoka kampuni ya Mikono Speakers na Mikono Expo Group ametolea mfano nchi kama ya Afrika Kusini kuna sheria zinazoongoza sekta ya Maonesho ili kuingia kwenye sekta hiyo ni lazima ufikie viwango vyao hii hupelekea kudhibiti ubora hivyo kama nchi kuna uhitaji wa kudhibiti Maonesho ili kumlinda mshiriki, sekta na hadhi ya nchi kwa ujumla.

Bi. Cresensia Mbunda kutoka Chemba ya Wanawake Tanzania (TWCC) amesema
kuwepo kwa sheria na kanuni ni mfumo mzuri ambao utawasaidia wafanyabiashara kwa ujumla hasa wanawake kwa kufuata maelekezo sahihi kwasababu wapo waliopata shida kutokana na mapungufu ya waandaji wa Maonesho mbalimbali.

Pia, Bw. Dominic Shoo kutoka kampuni ya Kili Fair Promotion Co Ltd ameunga mkono na kueleza kumekuwa na Maonesho ya aina nyingi nchini na kupelekea watu kuhangaika mara kwa mara, hivyo udhibiti wa Maonesho nchini yatampa Mtanzania kile anachokitarajia kutoka kwa muandaaji maana yataleta tija kwasababu Maonesho yanatangaza nchi pia

Majukumu ya TanTrade kisheria kifungu cha 5 cha Sheria Na. 4 ya 2009
kimeorodhesha Majukumu mbalimbali ya TanTrade kwa Umma. Kwamfano, kuhusiana
na Maonesho yanayofanyika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kifungu cha
5(1),(b) cha Sheria hiyo kama ilivyorekebishwa Na. Sheria Na. 3 ya 2012 kinaipatia
TanTrade mamlaka ya kuunganisha na kudhibiti Soko la Ndani, Maonesho ni sehemu
ya utekelezaji wa kifungu hicho. Kanuni ya 3(1), (k) ya kanuni za TanTrade za 2010
kinaipatia mamlaka TanTrade ya kutoa Vibali mbalimbali kwa Waandaji wa Maonesho
nchini.

Aidha, Kifungu cha 5(1), (p) cha Sheria hiyo, kama kilivyorekebishwa na Marekebisho
ya Sheria Na.3 ya 2012 kinaipa TanTrade mamlaka ya kumruhusu mtu yeyote au
Taasisi au Shirika kuandaa Maonesho ya Kimataifa ndani na nje ya nchi. Sheria pia
inabainisha uwepo wa Adhabu mbalimbali iwapo kutatokea ukiukwaji wake