************************
Na Silvia Mchuruza.
Kagera.
Katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari zaidi ya vyumba 570 vya maabara vinaitaji ili kuwanufaisha wanafunzi kati ujifunzaji kwa vitendo.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa Bw.Mbaraka Maya wakati akiwasirisha taarifa ya maendeleo ya elimu katika mkoa amesema kuwa vyumba vya maabara vilivyopo katika shule za sekondari ni 268 na ndivyo vinavyotumika.
Amesema kuwa juhudi zinaendelea kukamilisha vyumba vya maabara 352 vinavyopungua ambavyo viko katika hatua mbalimbali za ujenzi kutokana na kuwepo kwa upungufu wa miundombinu katika shule.
“Halmashauri zimetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha miundombinu inayopungua na waheshimiwa wakuu wa wilaya walishaelekezwa kusimamia suala hili” alisema Bw.Mbalaka.
Hata hivyo aliongeza na kusema kuwa hali yakiwango cha taaluma na ufaulu wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kimekuwa kikiimarika kila mwaka ambapo katika upimaji wa kitaifa wa Datasa la nne (SFNA) mwaka 2017 na 2018 mkoa wa kagera umeshika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka miwili mfululizo ufauli ulifikia asilimia 98.1.
Aidha alisema kuwa katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ufaulu uliongezeka mwaka 2017 kwa asilimia 84.2 na 2018 ilikuwa asilimia 84.4 ambapo mkoa ulishika nafasi ya tano kitaifa.
Sambamba na hayo nae mkuu wa mkoa kagera Brigedia General Marko Erisha Gaguti amezipongeza juhudi za sekta ya elimu mkoani humo mbali na kuwa na changamoto za maabara upande wa sekondari.
Ambapo kwa upande wa elimu ya msingi kwa mwaka 2019 ufaulu umeongezeka pia na kufikia asilimia 88.11 na kuufanya mkoa kuwa wa 4 kitaifa.