***********************
NJOMBE
Wakazi wa Kijiji cha Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu na kuhara kufuatia kutapakaa kwa vinyesi katika kaya nyingi katika kijiji hicho ambacho kimetajwa kuwa na wakazi wasio na utamaduni wa kujenga vyoo na kuamua kujisaidia porini.
Hofu hiyo imetolewa na mkurugenzi wa shirika la People Development Forum(PDF) nchini Ndaisaba George Nduguru katika semina ya siku mbili ambayo imekutanisha kamati za afya mkoa,Madiwani,wakurugenzi pamoja na maafisa tarafa kutoka halmashauri 6 za mikoa ya Mbeya ,Iringa na mwenyeji Njombe kwa lengo la kupeana uzoefu katika utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira.
Akizungumzia hali hiyo mkurugenzi huyo amesema kabla ya kukutana katika mafunzo hayo yakujengeana uwezo NGO’S hiyo ililazimika kufanya ziara ya kushitukiza katika maeneo mbalimbali katika wilayani ya Makete na kujionea kaya nyingi za kijiji cha Lupalilo zikiwa hazina vyoo huku makazi yakiwa yametapakaa vinyesi hatua hatua ambayo inahatarisha usalama wa wananchi na kuhitaji jitihada za lazima kuchukuliwa dhidi ya hali hiyo.
Katika hatua nyingine Ruholo amesema kiwango kikubwa cha udumavu pia kimekuwa kikisababishwa na uchafuzi wa mazingira pamoja na mlo huku takwimu zikionyesha kila penye watatu 3 mtoto 1 anaudumavu hivyo kila mmoja anapaswa kuhakikisha anasafisha mazingira pamoja choo bora .
Mtandao huu umefanya mahojiano na Bonifas Sanga ambaye ni mratibu wa kampeni ya usafi wa mazingira na afisa afya wilani Makete anakanusha uwepo wa hali hiyo katika kata ya Lupalilo kijiji hapo na kuitaja kata ya Kipagalo kuwa ndiyo kata pekee yenye changamoto ya vyoo katika kaya 6 ambazo zinakaliwa na wazee.
Mara baada ya mefunzo washiriki wanalazimika kwenda katika baadhi ya vijiji ambavyo vimefanikiwa kutekeleza kampeni ya usafi wa mazingira kwa asilimia 100 katika halmashauri ya wilaya ya Njombe kikiwemo kijiji cha Matiganjola, Image,Kidegembie na Ikuna ambapo siri ya mafanikio hayo inawekwa bayana na wakazi wa vijiji hivyo kwa wageni wao ambapo wanasema walitunga sheria ndogo ili kuwachukulia hatua wanaopuuza kampeni.