**********************************
EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba leo imeendeleza kutoa kichapo kwenye ligi kuu Vodacom ambapo leo hii imeinyuka timu ya Azam 1:0.
Mchezo huo ambao ulipigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kulishuhudia mchezo huo ukiwa mchakamchaka hasa timu zote zikiwa zinashambuliana.
Simba wakiwa wenyeji wa mchezo iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 49 kuandika bao la kuongoza lililopachikwa kimiani na Kagere akimalizia pasi ya Francis Kahata kwa kichwa.
Ushindi huo unaifanya Simba kuzidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 15 na imecheza michezo mitano kwa kusepa na pointi zote tatu.
Beki wa Simba, Pascal Wawa ndiye alikuwa nyota wa mchezo kwani aliokoa hatari nyingi kutoka kwa Chirwa ambaye alikuwa msubufu langoni akihaha kupata goli la ushindi ila bahati haikuwa yao.