Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina ya Wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region) itakayofanyika Jijini Arusha, tarehe 26 – 29 Oktoba, 2019, leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Kushoto ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya chama Cha wabunge wanawake wa mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Afrika Region).
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, amesema chama hicho kimeandaa semina na lengo la semina hiyo ni kuwahamasisha wajumbe wake mambo mbalimbali hasa katika kushiriki katika masuala ya uchaguzi.
“Chama Cha wabunge wanawake wa mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kimeandaa semina ya kuwahamasisha wajumbe wake kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu wanawake hususa ni katika eneo la uchaguzi,”
“Semina hii itafanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Oktoba 2019, Jijini Arusha, na kuwa na washiriki takribani 50 kutoka katika nchi 18 za Jumuiya ya Madola miongoni mwa nchi hizo ni Afrika Kusini, Botswana, Cameroon, Eswatini na nchi nyingine” amesema Spika Ndugai.
Semina hiyo itakayo bebwa na kauli mbiu ya “Kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi” pamoja na Mambo mengine ni kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi.
Ametaja miongoni mwa maada zitakazojadiliwa ni “Bulding Democracy Through Women participation in electoral processes as voters and Candidates, Barriers against women participation in elections, Violence and discriminatory practices against women during elections and Women Politicians and media : post- election engagement” amesema.
Aidha amesema miongoni mwa wageni watakaohudhuria ni Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na Mabalozi wa nchi 17 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya madola, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Balozi wa Pakstani, Mawaziri na viongozi wanawake, viongozi wa dini na wawakilishi kutoka UN Women Tanzania.
Pia amebainisha kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio makao makuu ya Chama Cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, ambayo inawabunge wanachama kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Madola zilizopo katika bara la Afrika na mabunge mengine 46 ya majimbo kutoka Afrika kusini 9, Nigeria 36 na Tanzania 1.