Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikata utepe kuzindua vitabu vya Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo, leo tarehe 21 Octoba 2019. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Dkt Anna Mghwira na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) Ndg Aloyce Mdalavuma (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la kahawa linalomilikiwa na Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) wakati alipotembelea makao makuu ya Taasisi hiyo Lyamungo Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 21 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikata utepe kuzindua vitabu vya Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo, leo tarehe 21 Octoba 2019 eneo la Lyamungo Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikabidhiwa zawadi ya Kahawa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) Ndg Aloyce Mdalavuma mara baada ya kuzindua vitabu vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo, leo tarehe 21 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Dkt Anna Mghwira na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Khatib Kazungu wakikagua shamba la kahawa linalomilikiwa na Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) wakati alipotembelea makao makuu ya Taasisi hiyo Lyamungo Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 21 Octoba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro
Moja ya changamoto
katika kuimarisha ubora wa Kahawa ni uzalishaji mdogo ya Miche ya Kahawa huku
mahitaji yakiwa ni makubwa kwa wakulima.

Wizara ya Kilimo
imekusudia kuzalisha mbegu mpya ambazo ni bora za kahawa kwa lengo kubwa la
kubadilisha mikahawa ya zamani ipatayo milioni
240 kwa kutumia aina mpya za kahawa.

Waziri wa Kilimo
Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 21 Octoba 2019 wakati wa
uzinduzi wa vitabu vya kanuni bora na mitaala ya ufundishaji katika zao la
Kahawa katika Ofisi za Taasisi ya utafiti wa Kahawa TACRI Wilayani Hai Mkoani
Kilimanjaro.

Alisema kuwa
uzalishaji wa idadi ya miche milioni
saba (7) kwa mwaka ni kidogo, ambapo itatuchukua takribani Miaka 35 kubadili aina hizi za zamani
hivyo aliahidi kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo itahakikisha
kunakuwa na mapinduzi ya Kilimo cha kahawa nchini.

Katika kuifikia
dhamira ya kubadili mikahawa ya zamani serikali kupitia wizara ya kilimo
imejipanga kuanza kuzalisha Miche milioni 20 ya kahawa mpya ili kuongeza tija
na uzalishaji wa kahawa.

Amesema
kuwa sekta ndogo ya kahawa ina umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa taifa na
huchangia takribani asilimia 24 kwa
mwaka ya mapato ya mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi, ambapo ni wastani wa asilimia 4 ya pato la taifa.

Hata
hivyo, pamoja na mchango huo wa sekta ndogo ya kahawa uzalishaji bado ni mdogo
sana, ambapo kwa mwaka wastani wa tani 50,000 huzalishwa.

Aliongeza
kuwa hali hiyo inasababishwa na tija ndogo ambapo mpaka sasa mti mmoja wa
kahawa unatoa gramu 250 ikilinganishwa na wastani wa gramu 1,000 inayotakiwa
kuvunwa kwa mti.

Moja
ya changamoto inayosababisha tija kuwa chini katika sekta ndogo ya kahawa ni
ukosefu wa elimu ya kanuni bora ya kilimo cha kahawa kwa wakulima ambapo
amewataka maafisa kilimo kote nchini kuanza kutoa elimu kwa wakulima juu ya
umuhimu wa mikahawa mipya.

Alisema ili kuhakisha kuwa mkulima anapata tija kubwa
na kuongeza kipato kutokana na kilimo cha kahawa, ni muhimu kupata elimu ya
uzalishaji wa kahawa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya kanuni bora za kilimo
cha kahawa.

Waziri Hasunga ameipongeza TaCRI kwa kuandaa vitabu vilivyozinduliwa
kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya
Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo ambavyo vitatumika kwa Maafisa Ugani,
Wakulima na Wananchi wote wenye nia ya kujifunza mbinu bora za kilimo cha
kahawa chenye tija.

Mhe Hasunga amesema kuwa Vitabu hivyo vyenye picha na
maelezo ya kutosha vimelenga kuwapa wakulima wa kahawa utaalamu wa kukuza zao la
kahawa katika lugha rahisi ambapo lengo la vitabu hivyo ni kuhakisha kuwa kaya
za wakulima wa kahawa zipatazo 420,000
nchini; wanakuwa na rejea ya haraka na rahisi wakati wote wawapo shambani,
mahali ambapo hawana wataalamu; na pale ambapo kutakuwa na mtaalamu vitakuwa vichocheo
vya mazungumzo ili kuweza kujua zaidi au kupata ufafanuzi wa kitaalamu wa
masuala ya kilimo cha kahawa.