Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Shelui Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe akizungumza na wazazi katika mahafali hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika shule hiyo mkoani Singida.
Mbunge Mattembe akisalimiana na mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Elly Nguma. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Shelui Kinota Hamisi, Afisa Elimu Kata Swetu Makula na Diwani wa Viti Maalumu wa Kata hiyo, Jenipher Miano.
Bweni la wanafunzi wa kike ambalo ujenzi wake ukiendelea.
Mhe. Mattembe akizungumza na viongozi wa kata hiyo wakati akikagua ujenzi wa bweni la wasichana wa shule hiyo ambalo serikali ilitoa sh. milioni 75.
Mattembe akizungumza na viongozi wa kata hiyo wakati akikagua ujenzi wa bwalo la shule hiyo ambapo serikali ilitoa sh.milioni 100.
Mhe.Mattembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kata hiyo mbele ya bwalo hilo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhe.Mattembe akiwasalimia kwa kuwapungia mikono wahitimu katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Kasimu Maksudi akizungumza katika mahafali hayo.
Mkuu wa shule hiyo Elly Nguma akizungumza.
Afisa Mtendaji Geofrey Tungu akizungumza.
Vijana wa Skauti wa Shule hiyo wakiingia katika viwanja vya mahafali kwa ukakamavu.
Vijana wa Skauti wa Shule hiyo wakionesha sarakasi.
Skauti wakionesha umahiri wa kuvunja tofari juu ya tumbo kwa kutumia nyundo.
Wahitimu wakiimba wimbo maalumu.
Mhe.Mattembe akiserebuka na wanamuziki wa kizazi kipya wa shule hiyo.
Wahitimu hao wakiigiza kuimba na kucheza muziki wa wazee wa zamani.
Keki maalumu ya mahafali hayo.
Mhe.Mattembe akikata keki hiyo.
Wananchi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wananchi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhe.Mattembe akilishwa keki hiyo.
Mahafali yakiendelea.
Taswira ya uwanja wa mahafali hayo.
Mhe.Mattembe akimkabidhi cheti cha Taaluma Mhitimu, Hassan Juma.
Mhe.Mattembe akikabidhi jezi na mpira kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Hapa Mattembe akikabidhi taulo kwa ajili ya watoto wa kike wa shule hiyo.
Mhitimu Agnes Daudi akionesha kipaji cha kuimba.
Wazazi wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa mchango wa ujenzi wa bwalo la shule hiyo baada ya kuhamasishwa na Mbunge Mattembe.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Viongozi na wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Viti Maakumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amewataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kujitokeza kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo badala ya kuiachia serikali pekee.
Mattembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Shelui alitoa ombi hilo wakati akihutubia kwenye mahafali hayo.
“Serikali ina majukumu mengi katika nchi nawaombeni wazazi na walezi jengeni tabia ya kuchangia miradi ya maendeleo ili kuisaidia serikali” alisema Mattembe.
Mattembe alisema katika shule hiyo kuna miradi ya ujenzi wa bwalo na bweni la wanafunzi wa kike ukiendelea lakini umekuwa ukisuasua baada ya fedha zilizotolewa na serikali kumalizika hivyo aliwaomba wazazi hao kuchangia ujenzi huo ili kuwapunguzia adha watoto wao ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.
Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutawaongezea ufaulu wanafunzi wa shule hiyo kwa vile watapata muda wa kutosha wa kujisomea.
Mattembe aliwataka wazazi hao kuwa na muda wa kuzungumza na watoto wao mambo mbalimbali ya kuwajenga katika misingi mizuri ya maisha badala ya kuwaacha wakiharibikiwa kwa
kujiingiza katika vitendo viovu.
Katika hatua nyingine Mattembe aliwaomba wazazi hao kuviendeleza vipaji walivyo navyo watoto wao vya kuimba, kuigiza na michezo mbalimbali na kueleza kuwa vinawajenga na
kuacha kufikiria mambo yasiofaa.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Kasimu Maksudi aliwaeleza wahitimu hao kujiandaa kwa mtihani wao wa mwisho na kuwa kuhitimu kwa kidato cha nne ndio mwanzo wa kuendelea na
masomo mengine ya kidato cha tano na sita hadi elimu ya juu hivyo wasibweteke kwa kuridhika na elimu hiyo.
Kabla ya kuhutubia katika mahafali hayo Mattembe alikagua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana ambao serikali ilitoa sh. 75 milioni na sh. 100 milioni kwa ajili ya bwalo.