Home Mchanganyiko MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA...

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR.

0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.Bi. Lela Burhani Ngozi, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo 20-10-2019 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa meza kuu (kulia kwa Rais) Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, wakipitia makabrasha ya Kikao cha Kamati Maalum ya CCM,wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kabla ya kuaza kwa Kikao hicho.(Picha na Ikulu)MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na kufungua Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kulia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu).

 

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo Tarehe Octoba 20,2019  ameongoza Kikao Maalumu cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho cha siku moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe  wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

Kupitia Kikao hicho Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kikao hicho ni mwendelezo wa kujadili baadhi ya ajenda zilizotokana na kikao kilichopita ambazo zilitakiwa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Kikao hicho.

Kikao hicho ni maalumu kinachojadili masuala mbali mbali ya Chama kwa  mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977 Toleo jipya la 2017.

Viongozi mbali mbali Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’.