Wafanyabiashara Wakubwa kutoka katika nchi mbalimbali wakijadili ni namna gani wanaweza kushirikiana kwa pamoja katika kukuza biashara katika sekta ya Utalii
************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wafanyabiashara wakubwa kutoka katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi wamekutana kwa pamoja na kujadili ni namna gani wanaweza kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kukuza biashara katika sekta ya Utalii.
Akizungumza katika Onesho la Kimataifa la Swahili la Utalii (SITE), Katibu tawala msaidizi sekta ya uchumi na uzalishaji Mkoa wa Iringa Bw.Elias Luvanda amesema kuwa tutegemee kuongezeka kwa utalii hapa nchini pamoja na biashara kupanuka hivyo hata wafanyabiashara wakawaida wataweza kunufaika kupitia watalii.
“Tujivunie katika onesho hili kwani maendeleo yapo tumeona maudhulio yamekuwa mazuri hivyo tutegemee vitu vizuri kupitia onesho hili”.Amesema Bw.Luvanda.
Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa kampuni ya usafirishaji Watalii Zanzibar Sun Tours and Travel,Bi.Tetula Okama amesema kuwa wanategemea kupata ushirikiano mkubwa kupitia wageni kwani wakifanya hivyo hata biashara zao hususani katika sekta ya utalii utakua pamoja na kuongezeka kwa pato la taifa.
“Kupitia hawa wageni watatusaidia kututangazia biashara zetu kupitia sekta Utalii katika nchi zao hivyo kutaongezeka kwa idadi ya watalii hapa nchini”. Amesema Bi.Tetula.