………………
Na Mwandishi Wetu Hanang Manyara
Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuondoa umasikini duniani huku ikisemekana kuwa watanzania walio wengi wanakabiliwa na umasikini wa kifikra zaidi kwa kukosa kutambua firsa za kimaendeleo unaosababisha kuleta umasikini wa kipato.
Hayo yamebainika wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya siku tatu mfululizo ikiwa ni Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini,Siku ya Chakula Duniani na Siku ya kuondoa Umasikini Dunaini yaliyofanyika katika Kijiji cha Gehandu Wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara yaliyoratibwa na Wizara ya Afya, Idara Kuu ya MAendeleo ya Jamii.
Akizungumza wakati wa hitimisho ya maadhiisho hayo Mkuu waWilaya ya Hanang Mhe. Joseph Mkirikiti amesema kuwa watanzania waliowengi wanasumbuliwa na umasikini wa kifikra zaidi unaopelekea umasikini wa kipato.
“Nitolee mfano katika Wilaya ya Hanang utakuta katika jamii sio watu wanakosa pesa ila ni kukosa kutambua fikra za kuweza kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato” alisisitiza Mhe. Mkirikiti
Ameongeza kuwa jambo kubwa linaloanisha umasikini ni ukosefu wa fursa za kimaendeleo kwa jamii nyingi za kitanzania hivyo elimu inahitajika kwa wananchi hasa wa vijijini hasa katika kutambua fursa za kimaendeleo na kuzifanyia kazi.
Mhe. Mkirikiti amesema kuwa kwa upande wa Wilaya ya Hanang umasikini wa kipato haupo ili kuna hitajika elimu wananchi ya jinsi ya kutumia fursa za kimaendeleo kwa kutumia kipato wanachopata kujileta maendeleo kwa kujenga nyumba bora na kupeleka watoto shule.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mratibu wa maadhimisho kutoka Wizara hiyo Bi.Silyvia Siriwa amesema kuwa mwanamke akiwezeshwa kiuchumi na kuondokana na umasikini ana uwezo wa kulea familia na kupunguza masuala ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.
“Sisemi kama wanaume hawalei familia ila mwanamke akiwa na uwezo wa kiuchumi kwa kiasi kikubwa anaweza kuiangalia familia kwa ukaribu hasa katika malezi ya watoto” alisema Bi. Silyvia.