***********************
Na Silvia. A. Mchuruza.
Mkuu wa Wilaya karagwe Mh Godfrey Mheruka ametoa wito kwa jamii kuwachukua watoto wote kuanzia watoto wenye umri wa miezi tisa mpaka miaka minne kuwapeleka kwenye vituo vya kutolea chanjo ya sulua rubela ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.
Mh Godfrey Mheruka ametoa wito huo hii leo kwenye uzinduzi wa chanjo ya sulua lubela kwa niamba ya mkuu wa mkoa kagera Brigedia Elisha Mariko Gaguti iliyo zinduliwa kimkoa katika viwanja vya kituo cha afya Kayanga wilayani Karagwe.
Mh mweruka kabla ya kuzindua chanjo amemtaka msimamizi wa chanjo hiyo kimkoa Dr Deliphinus Mjuni kutoa semina kwa wananchi walio kuwa wamekusanyika katika viwanja hivyo.
Pia Mh mweruka amewahakikishia wananchi kwamba chanjo hiyo haina madhara yoyote na wananchi wasisite kupeleka watoto wao kwani serikali imejihakikishia kuwa ni salama kwa watoto wote walio legwa.
Naye mmoja wa akina mama Bi Mukamala Byamungu ambaye mtoto wake alipatiwa huduma hiyo hivi karibuni amewahasa wakina mama wenzake kutokuwa na imani potofu juu ya chanjo hiyo iliyozinduliwa nakusema kuwa haina madhara kwa afya ya motto.Chanjo ya surua lubela ambayo imezinduliwa leo tarehe 17 inatarajiwa kuhitimishwa tarehe21 Octoba mwaka huu