Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasi na Utalii, Prof.Aldof Mkenda(Katikati)akiongea na Waandishi wa habari baada ya kutoa taarifa kuhusu Onesho la Utalii la Kimataifa la Swahili (SITE) Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi akiongea na Wanahabari baada ya utoaji taarifa kuhusu Onesho la Utalii la Kimataifa la Swahili (SITE) Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO
Zaidi ya Kampuni za Waoneshaji 210 kutoka nchi 60 na jumla ya wakala wa utalii wa kimatifa na waandishi wa habari takribani 333 wanatarajia kushiriki katika onesho la utalii la Kimataifa la Swahili (SITE) Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasi na Utalii, Prof.Aldof Mkenda amesema kuwa Katika ufunguzi wa Onesho hilo kunatarajiwa mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Pombe Magufuli.
Aidha, Prof.Mkenda ameishukuru ofisi za Ubalozi nje ya nchi kwani zimefanya kazi kubwa ya kufanya usaili wa Mawakala wa Utalii pamoja na waandishin wa habari watakaoshiri kutoka nchi wanazosimamia.
“Ofisi zetu za ubalozi ambazo wamefanya kazi nzuri sana ya kusaidia kuleta mawakala wapatao 142 kutoka jumla ya nchi ishirini na mbili (22) ambapo ubalozi wa Tanzania nchini Swede ambao umeleta washiriki kutoka nchini Sweden, Norway,Finland,Denmark,Latvia,Estonia,lithuania, pamoja na Ukraine. Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia ambao umeleta washiriki kutoka nchi za Malaysia, Thailand, Philipines, Indonesia pamoja na Brunei. Ubalozi wa Tanzania nchini China na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini”.Amesema Prof.Mkenda.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi amesema kuwa katika onesho hilo litakaloanza kufanyika kesho Oktoba 17, wamepata udhamini kutoka mashirika na makampuni ya Umma zaidi ya 98 ambayo wamewadhamini kwa namna mbalimbali.
“Kwa kuwa makampuni ni mengi ikiwa ni pamoja na The Global Vector Control Standard, Benki ya CRDB, HANSPAL Companies, Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), Kampuni ya mafuta ya Total Excab, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), Most Hired International, Emirate Airlines,Auric Air, Flight Link na G$S Security Company. Hayo ni baadhi ya Makampuni Makubwa”. Amesema Bi.Devota.