Home Mchanganyiko WAITARA AWAONYA WATUMISHI WA SEKTA YA ELIMU KUTUMIA FEDHA VIBAYA KAGERA.

WAITARA AWAONYA WATUMISHI WA SEKTA YA ELIMU KUTUMIA FEDHA VIBAYA KAGERA.

0

********************************

Na Silvia Mchuruza, 
Bukoba
Naibu Waziri wa Tamisemi Mheshimiwa Mwita Waitara amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa kwenda chini kusimamia fedha za Serikali ambazo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kila chumba cha darasa mbapo takribani shilingi  milioni 12.5 zimetumika.
Naibu Waziri Waitara ameyasema hayo leo akiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa  Kagera baada ya kufika mkoani hapa kwa kwaajili ya ziara ya kikazi kwa siku nne.
Amesema, katika kukamilisha chumba cha darasa ambacho jamii inakuwa tayari imeishaweka nguvu zake hadi usawa wa lita serikali inachangia 12.5 milioni kwa ajili ya vifaa vya viwandani ili kukamilisha ujenzi wa chumba hicho.
Aidha,Mh.Waitara ameongeza wazazi lazima  washirikiane na serikali pale wanapotakiwa katika  swala la elimu na kuwa viongozi kupitia bodi za shule wawambie wananchi kuwa michango inaruhusiwa kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu.
“Katika kutoa elimu lazima tushirikiane wazazi  na serikali na michango inaruhusiwa kwa utaratibu ambao uliwekwa na serikali ambao hauwahusishiwalimu kupokea michango hiyo”. Amesema Mh.Waitara
Kwa upande wake afisa elimu Mkoa wa Kagera Bw.Juma Mhina ameeleza kwamba, serikali imetoa shilingi bilioni moja katika Mkoa wa Kagera kwa ajili ya vyumba vya madarasa shule za msingi na shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za sekondari.