………………………
Na Farida Saidy Morogoro
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na wale wanaofanya kazi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo wameaswa kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu kwa kuwa hiyo ndiyo silaha pekee kwa Mtumishi wa Umma.
Haya yamesemwa Oktoba 15 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare alipokuwa anazungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mwendelezo wake wa kujitambulisha kwa kila Halmashauri na kuzungumza na watumishi ili kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Amewataka watumishi hao kusimama imara katika kufanya kazi na kutumia weledi wao kwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kwamba uadilifu ndiyo silaha muhim katika kufanya kazi ya Umma.
“Uadilifu katika kufanya kazi ni kitu kizuri sana, msishangilie kwa sababu mmeona wengine na kweli walimopita mmeona kilichotokea, sasa aje hapa akute tuko wamoja na tunachapa kazi” alisema Mhe. Sanare.
Hata hivyo Mhe. Sanare anaendelea kuwakumbusha watumishi wote wa Umma kutumia vema rasilimali za Serikalizilizopo iwe fedha za kutoka Serikali Kuu ama fedha zinazokusanywa na Halmashauri.
Amesema mtumishi atakayetumia vibaya rasilimali hizo atahesabika adui namba moja wa Serikali na Halmashauri anayofanyia kazi huku akibainisha kuwa mtumishi wa aina hiyo kamwe hatohamishwa badala yake ataachishwa kazi, hilo likiwa pia ni agizo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo MHe. Mwalimu Mohamed Utali kuwaweka kando wabadhirifu wote wa mali ya Serikali ndani ya Wilaya yake.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kufanya kazi kwa Ufasaha, kwa Ufanisi na kwa wakati na kwamba hayo yatawezekana tu pale mtumishi atakapoamua kufanya kazi kwa uwazi.
Akiwajengea kujiamini zaidi Mhandisi Kalobelo amewataka watumishi hao kujijengea tabia hiyo ya uwazi itamsaidia kushirikisha wengine pale anapokutana na changamoto katika utekelezaji wa majukumu yake.
Amesema ni jambo jema kwa Mtumishi wa Serikali kumshirikisha kiongozi wake mapema au mtumishi mwenzake yeyote ili kusaidiwa changamo anayokumbana nayo badala ya kubaki nayo kwa muda mrefu na ri utendaji wake wa kazi na wa taasisi yake.