Na Farida Saidy Morogoro
Watu Tisa (9) wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti wakiwemo wanafunzi watano wa shule ya Msingi Nyachiro waliozama Mtoni walipoenda kuogelea, baada ya kuzidiwa na Maji yaliyo tokana na mvua zinazo endelea kunyesha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa amesema tukio la wanafunzi kufa maji limetokea Oktoba 12 majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha Nyachiro Tarafa ya Matombo.
Katika hatua nyingine Ngeze Mwagilo mfanyabiashara mkazi wa kasanga manispaa hii ya Morogoro anashikiliwa na Polisi akidaiwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura katika vituo viwili tofauti.
hata hivyo jeshi la polisi limewasisitiza wananchi kuwa makini na kuweka uangalizi wa karibu kwa watoto wao, hasa katika kipindi hiki mvua zinavyo endelea kunyesha.
Pamoja na mambo mengine wakazi wa Morogoro wametakiwa kuendeleza ushirikiano kuwafichua wanaojihusisha na uvunjifu wa amani, sambamba na kutakiwa kuendelea kufanya kazi halali za kujiingizia kipato.