***************************
NJOMBE
Mamia ya wananchi wameshiriki matembezi katika viunga vya mji wa Njombe ambayo yameandaliwa na halmashauri ya mji wa Njombe kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Mbali na kuhamasisha zoezi la uandikishaji lakini pia halmashauri hiyo imetumia matembezi hayo kama kumbukizi ya kifo cha miaka 20 cha baba wa taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere.
Awali akizungumza katibu tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George pamoja na msimamizi wa uchaguzi hamashauri ya mji wa Njombe Venance Msungu wanasema wamelazimika kutumia mbinu ya kufanya matembezi katika viunga vya mji wa Njombe pamoja mazoezi ya pamoja ili kutoa hamasa kwa umma kujitokeza kujiandikisha .
Fullshangwe imezungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Njombe ambao wameshiriki katika matembezi hayo akiwemo Wilton Mwaisela na Yasinta Kisima wanaeleza jinsi walivyo hamasika kujiandikisha na kutoa rai kwa wengine kushiriki.