Na.Imani Kelvin Mbaga,Dar es Salaam
Mnamo tarehe 18 Machi mwaka 1900, ilianzishwa klabu ya mpira wa miguu iliyotikisa ulaya kwa miongo kadhaa, ikiwa na miundo mbinu, historia na mafanikio ya kujivunia, ikiitwa Ajax Amsterdam huko nchini Uholanzi.
Hii ni klabu ambayo imekuwa mhimili wa soka la Uholanzi na bara la Ulaya kwa kipindi kirefu.
Ajax ambao wamewahi kubeba ubingwa wa Uholanzi mara 34, kombe la Uholanzi (KNVB) 19, kombe la Ulaya/ ligi ya mabingwa 4, kombe la washindi Ulaya 1, kombe la ulaya 1, super cup 2, na makombe mengine mengi.
Klabu hii inajulikana kwa kuwa na kituo bora cha kukuzia vipaji (shule ya michezo) maarufu kama “Ajax youth Academy” ambayo ina jumla ya timu 13 za watoto wenye umri kati ya miaka 7-18.
Kituo hiki cha michezo wamepitia nyota zaidi ya 40 wa soka wakiwemo Johan Cruijiff, Frank Rijkaard, Dennis Bergkamp, Edga David’s na wengine wengi ambao si tu walikuwa ni nguzo ya soka la Uholanzi hasa timu yao ya taifa bali pia nguzo ya vilabu mbalimbali ikiweno fc Barcelona ya nchini Hispania.
Miamba hiyo ya soka imekuwa ni moja ya klabu muhimu sana kwa bara zima la Ulaya.
Misingi ibayoibeba klabu hii ni
– Maono
– Mipango
– Mikakati
– Weledi
Imejijengea misingi yake na kuifuata, bila kuyumbishwa na mabadiliko ya wakati, fikra au mitazamo. Waliamua kuwa na utamaduni wao, wakauamini, wakauheshimu, wakaamua kuutunza na kuufuata.
Hii ni klabu inayoongozwa ba watu waliojaa weledi ambao wanajua misingi ya utamaduni na mwelekeo wa klabu na wanaifuata kikamilifu.
Hapa kwetu ipo timu ya Azam iliyopo jijini Dar es salaam na Alliance iliyoko jijini Mwanza ambapo hizi ni timu ambazo nikiziangalia zina mlingano na Ajax katika wazo lkn nadhani shida ipo kwenye misingi na makusudi yao.
Waanze sasa kwani hawajachelewa, watengeneze sera maalumu itakayokuwa tamaduni za klabu zao, waweke mipango mahsusi ya muda mfupi na mrefu, watafute ushauri wa kitaalamu toka kwa walioendelea, waajiri wataalamu waliobobea ikiwezekana toka nje ya nchi mwisho waheshimu mipango yao bila kuruhusu siasa za soka letu kuwaathiri.
Nategemea Azam na Alliance kuwa nguzo ya soka la Tanzania, Afrika na duniani kwa jumla, kwakuwa mafanikio ya Ajax ni barua ya wazi kwao