Home Burudani Jaromax Hotel wadhamini shindano la Miss Utalii

Jaromax Hotel wadhamini shindano la Miss Utalii

0

Bi Gorgina Saulo Mkurugenzi wa Mashindano ya Miss Utalii Tanzania akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Jaromax Palace ya Tiptop Manzese jijini Dar es salaam leo wakati alipoitangaza hoteli hiyo kama mdhamini mkuu wa mashindano hayo mwaka huu.

Balozi wa Hoteli ya Jamarox Palace Bw.Batromeo Julius Makumbula akizungumzia ubora wa hoteli hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari na lengo kubwa la kudhamini shindano la Miss Utalii Tanzania.

Meneja Mkuu wa Hoteli ya Jaromax Bw. Thomas Fusi akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli hiyo jijini Dar es salaam leo.

Kaimu Afisa Habari wa baraza la Sanaa Tanzania BASATA Bw. Godfrey Nago akifafanua baadhi ya mabo kuhusu shindano hilo kwa upande wa BASATA.

…………………………………………….

NA MWANDISHI WETU

HOTELI ya kitalii ya Jaromax Palace iliyopo Tip top jijini Dar es Salaam imeingia makubaliano ya kudhamini shindano la Kimataifa la Miss Utalii Tanzania  2019/2020 na Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha shindano hilo nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano na Matukio wa Miss Utalii Tanzania Geogina Saulo udhamini huo ni wa Shilingi Milioni 152 ukijumuisha huduma za malazi, chakula, vinywaji na ukumbi wa mikutano na mazoezi.

Saulo alisema shindano hilo dhamira yake ni kukuza utalii Tanzania  ambako imekuja kivingine baada ya kuondoa kasoro zilizojitokeza miaka iliyopita.   

Alisema kwa kuanzia shindano hilo litafanyika kwa Kanda 8 ikiwemo Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza kwa visiwa hivyo kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Saulo alisema Miss Tourism International Peagant litashirikisha nchi zaidi ya 50, washiriki watatangaza vivutio vyetu.

Aidha Saulo alisema pia wamekuja na utalii uswahilini  watafanikisha matukio mbalimbali yanayofanyika uswahilini baadhi yake ni kama kupikia kuni kwa kupuliza moto kwa mdomo na ngoma za asili.

Mkurugenzi huyo alisema Oktoba 17 wanatarajia kufanya uzinduzi wa shindano hilo kwa sababu kabla ya shindano hilo kuanza wanarekebisha baadhi ya kasoro.

Meneja Mkuu wa hoteli hiyo, Thimas Fusi alisema wameguswa na tukio hilo baada ya kuona shindano hilo ndilo pekee litakaloiweka nchi kwenye ramani ya dunia.

Kaimu Ofisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Goefrey Nago alisema serikali inalifuatilia shindano hilo hatua kwa hatua kuzuia kasoro zilizojitokeza miaka saba iliyopita.

Nago alisema anaamini shindano hilo litakuwa bora zaidi ya lililopita kwa sababu wigo wake ni mpana zaidi kiutekelezaji.