Home Mchanganyiko DC IKUNGI AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI

DC IKUNGI AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI

0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akicheza sanjari na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mang’onyi Dayosisi ya Kati mkoani Singida katika mkutano wa kuliombea Taifa na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mtaa ulioandaliwa na kanisa hilo hivi karibuni. Kulia ni Mchungaji wa kanisa hilo, Emmanuel Kigolumbe.

DC Mpogolo akihutubia  katika mkutano huo.
Waumini wa kanisa hilo wakimtukuza mungu kwa kuimba na kucheza katika mkutano huo.
 
Mwenyekiti wa Kijiji cha  Mang’onyi Mohammed Ramadhan akizungumza kwenye mkutano huo.  

 Mchungaji wa kanisa hilo, Emmanuel Kigolumbe akizungumza kwenye mkutano huo.
 Watoto wakijumuika katika mkutano.
 Wakina mama wakiwa kwenye mkutano huo.
 Kiongozi wa kwaya ya Shalom Band, Samson Timotheo, akiwajibika.
Mkutano ukiendelea. 
Waumini wa kanisa hilo wakimtukuza mungu kwa kuimba na kucheza katika mkutano huo.
 DC Mpogolo akicheza katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 DC Mpogolo akiwa na viongozi wengine meza kuu.
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo amewata viongozia dini kuendelea kumuombea Rais Dkt.John Magufuli kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
 
Mpokolo alitoa ombi hilo hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa hadhara wa kuliombea Taifa na uchaguzi wa serikali za mitaa ulioandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Usharika wa Mang’onyi Dayosisi ya Kati mkoani Singida.
 
” Viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa ya kuifanya nchi yetu kuwa na amani na utulivu kutokana na kuiombea  na viongozi wake endeleeni kufanya hivyo na kumuombea Rais wetu kwani anafanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo katika nchi” alisema Mpogolo.
 
Mpogolo alisema Rais Magufuli ametekeleza miradi ya maji, umeme, ujenzi wa reli, vituo vya afya na zahanati zaidi ya 350, ununuzi wa ndege 11 katika sekta ya elimu ujenzi wa madarasa na kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari.
 
Aliongeza kuwa katika wilaya hiyo ametoa sh. 720 milioni kwa ajili ya kujenga kituo cha afya cha kisasa Kata ya Ihanja,  Kata ya Sepuka  sh.400 milioni, Kata ya Iyumbu sh. 500 milioni  na hospitali ya wilaya sh. Bilioni 1.500, 000,000 na kuwa  serikali imeanza kutandaza umeme wa Wakala wa Nishati ya Umeme Vijiji (REA) awamu ya tatu katika wilaya hiyo baada ya kusambaza nguzo.
 
Alisema kutokana na kazi hiyo kubwa anayoifanya Rais Magufuli anatakiwa  kuombewa ili awe na afya njema na kuendelea kuchapa kazi ya kuwatumikia wananchi.
 
Mpogolo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kujiandikisha na wale wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi ya uongozi wa vitongoji na mitaa katika uchaguzi utakaofanyika Novemba  24 mwaka huu.
 
” Kugombea nafasi za uongozi ni haki ya kila mtu  jitokezeni kugombea  na mimi sitanuonea huruma mtu yeyote atakaye jaribu kuvuruga uchaguzi huo kwa kuwatisha wananchi wakati wa upigaji kura” alisema Mpogolo.
 
Mchungaji wa kanisa hilo,  Emmanuel Kigolumbe alisema kuchagua viongozi wazuri ni jambo jema ambalo mungu analipenda na kuwa Rais Magufuli ni tawi la mzabibu litoae  matunda ambapo aliwataka waumini wa kanisa hilo na wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo ili kuwapata viongozi ambao wataunda serikali kuanzia ngazi ya vijiji na kuwa wawakilishi wao.