Baadhi ya wageni walioudhulia kongamano la miaka 20 bila baba wa taifa lililoandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi na kufanyika katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuuu cha Dar es Salaam.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, ameeleza namna serikali ya awamu ya tano ilivyotekeleza misingi ya maendeleo iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwemo ujenzi wa miradi ya kimkakati.
Hayo ameyasema leo wakati wa kongamano la miaka 20 bila baba wa taifa lililoandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi na kufanyika katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuuu cha Dar es Salaam.
Prof. Kabudi amesema kuwa Mwalimu Nyerere alihakikisha anaifanya lugha ya Kiswahili kutambulika na kila Mtanzania hivyo lugha hiyo ilitumuika katika ukombozi wan chi nyingi za Afrika hivyo kuifanya kutambulika Afrika.
“Haitoshi kuiita lugha ya Kiswahili kuwa tunu ya taifa bali hii ni lugha ya ukombozi wa taifa kwani mataifa mengi Afrika yamekombolewa yakitumia lugha hii,” alisema.
Alisema kwakuwa baba wa Taifa alifanya jitihada za ukombozi wa nchi za Afrika hivyo katika mapambano hayo alitumia lugha ya Kiswahili na kukifanya kutambulika Afrika nzima.
Akizungumza hali ya lugha hiyo kwa sasa Prof. Kabudi, amesema serikali ya awamu ya tano imefanya juhudi kubwa katika kuenzi lugha hiyo kama alivyotaka baba wa taifa na miongoni mwa mafanikio ya lugha hiyo kwa sasa ni pamoja na kuwa lugha ya kumi inayozungumzwa zaidi Duniani, kuanza rasmi kutumika katika mikutano ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.
“Tumepiga hatua kubwa sana katika kuenzi lugha ya Kiswahili maana mataifa mengine Rais akihutubia lazima awe na mkarimani maana yake si wananchi wote wanaotambua lugha anayotumia lakini Tanzania sote tunaitambua lugha ya Kiswahili,” Amesema Prof.Kabudi.
Hivyo Prof.Kabudi, amesema kuwa Mwalimu Nyerere, alipambana kila namna kuhakikisha haki ya elimu inamfikia kila mtanzania akiamini kuwa ndiyo chachu ya ukombozi wa taifa.
Aidha, Prof.Kabudi amesema kuwa katika kutambua hilo Mwalimu Nyerere alianzisha taasisi mbalimbali za elimu kwa watu wa kila rika ikiwemo elimu kwa watui wazima pamoja na kuanzisha vyuo kama kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Vilevile amesema kuwa tangu kuingia madarakani kwa Rais Dk. John Magufuli, alienzi msingi huo wa Baba wa Taifa kwa kuhakikisha kuwa elimu inapatikana na Mtanzania wa kila hali.
Hata hivyo ameongeza kuwa katika kufanikisha hilo serikali ya awamu hii inatenga zaidi ya sh. Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya kugharamikia elimu bila malipo kwa watoto wote nchini.
Pamoja na hayo Prof.Kabudi amesema kuwa fursa hiyo ya elimu imesababisha kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoandikishwa kujiunga na shule pamoja na kuongeza idadi ya ufaulu na hatimaye taifa kuwa na wasomi wengi.
Naye Makamu wa chuo kikuu Cha Dar es salaam (UDSM )Prof. William Anangise amesema kuwa kongamano hili limeandaliwa na kigoda cha kitaluma cha Mwalimu julias kambarage nyerere kwa kushirikiana na Taasisi ya uongozi miongoni mmwa Mada zitakatozo jadiliwa katika kujikita mambo ya Mwalimu Nyerere na pamoja na huduma za jamii.
Pia Prof.Anangise amesema kuwa chuo kina utaratibu kuandaa makongamano tofauti kama haya ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuweza kujadiliana maendeleo ya taifa.