Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akimwelekeza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye jinsi mfumo wa Instant School unavyofanya kazi, tumetoa Kompyuta mpakato 20, Router 10 na uunganishaji Inteneti kwa mwaka mzima kwa shule kumi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akizungumza na wageni waliohudhuria kwenye sherehe ya makabidhiano ya Kompyuta mpakato 20, Router 10 na uunganishaji Inteneti kwa mwaka mzima kwa shule kumi mkoani Simiyu.
………………………….
- Hii ni sehemu ya ajenda ya Vodacom ya kusaidia ukuwaji wa elimu kwa kupitia mfumo wa kidigitali nchini Tanzania.
8 Oktoba 2019, Simiyu. Kampuni inayoongoza ya Mawasiliano ya Vodacom PLC nchini Tanzania imetoa msaada wa kompyuta na kipanga njia (Router) zenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 48 pamoja na kuunganisha kwenye mtandao wa intaneti kwa shule kumi katika mkoa wa Simiyu kama sehemu ya mpango wake kusaidia ukuwaji wa sekta ya elimu.
Programu hii ni ushirikiano wa pamoja na Mfuko wa Huduma ya Mawasiliano ya (UCSAF) yenye lengo la kushinikiza ujumuishaji wa kusoma kwa mfumo wa kidigitali katika shule Tanzania. Kupitia ushirika huu shule 300 haswa vijijini zitapokea kompyuta na kuunganishiwa mtandao intaneti.
Akiongea katika shule ya Sekondari ya Simiyu mkoani Simiyu, Naibu Waziri wa Kazi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Atashasta Nditiye alisema mchango wa kompyuta unaenda mbali katika kuunga mkono agizo la serikali la kukuza maendeleo ya kijamii vijijini na mijini Tanzania kupitia mfumo wa mawasiliano.
“Vodacom imekuwa mshirika wa serikali katika maendeleo. Nina furahi kuona ushirika huu katika utekelezaji wa mradi wa serikali wa kuunganishwa kwa shule za uma nchini katika mfumo wa kidigitali. Tunashukuru sana kwa mchango huu na tunataka kampuni zingine kuiga zoezi hili katika kusaidia sekta ya elimu.”
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Foundation, Rosalynn Mworia alisema mpango huo ni sehemu ya ajenda ya kukuza mafunzo bora nchini Tanzania ambao unaelekea kufanikiwa kwa mipango ya maendeleo ya kimataifa. Kompyuta hizo pia zitawezesha shule hizo kuunganishwa mfumo wa upatikanaji wa elimu kwa njia ya kidigitali kupitia mtandao wa Vodacom.
“Tunafurahi kusaidia sekta ya elimu kama sehemu ya mpango wetu wa uwekezaji wa kijamii. Tumeshirikiana na serikali kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayesalia katika utimiaji wa mfumo wa kidigitali. Mbali na uchangiaji wa kompyuta, pia tunasaidia kila shule na kuunganishwa kwenye mtandao wa intaneti bure”. Mworia alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UCSAF Justina Mashiba alisema, “Tunajivunia kufanya kazi na Vodacom kuhakikisha mpango wetu unafanikiwa kwa kuunganisha shule zote za uma na upatikanaji wa mtandao ili kutumia kikamilifu vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano”.
“Mchango huu ni kusaidia kazi yetu ya kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kila mahali haswa katika jamii za pembezoni”.
Hafla hiyo ni sehemu ya awamu ya kwanza wa michango ya kompyuta inayotolewa na Vodacom Foundation na UCSAF kwa shule za uma nchini.
Vodacom imekuwa ikishiriki katika kusaidia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya habari shuleni kupitia mpango wake wa shule nzuri ambapo madawati 75 na kompyuta zilitolewa katika shule za sekondari ya Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja pamoja na shule ya sekondari ya Kinyerezi.
Ends
Kuhusu Vodacom:
Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawsiliano kwa zaidi ya wateja milioni 14. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu ya: www.vodacom.co.tz Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayoongoza kupitia taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa kompyuta kwa shule kumi mkoani simiyu ikiwa kama sehemu ya programu ya kuasaidia ukuwaji wa sekta ya elimu.