Home Uncategorized Mazao ya Wanyama kuongezeka zaidi ya mara mbili ifikapo mwaka 2020

Mazao ya Wanyama kuongezeka zaidi ya mara mbili ifikapo mwaka 2020

0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega akizungumza wakati akifungua Mdahalo juu ya vyakula vya asili ya wanyama na mchango wake katika masuala ya afya ya umma na lishe, na uzinduzi wa mikakati ya kitaifa ya kuzuia na kudhibti magonjwa ya brusela na kimeta kwa binadamu na wanyama uiofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili MUHAS jana jijini Dar es salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu kishiriki cha Afya Muhimbili  (MUHAS) Dk.Andrea Pembe akizungumza katika mdahalo huo  wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ili kufungua mdahalo huo.

Baadhi ya wa washiriki kutoka katika mdahalo huo kutoka chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili  MUHAS wakiwa katika mdahalo huo jana.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mifugo nchini Dkt. Hezron Nonga akitmdahalo huo.oa mada katika mdahalo huo

Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi akiwasilisha mada katika mdahalo huo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mifugo nchini Dkt. Hezron Nonga

………………………………………………

Naibu Waziri amesema takwimu kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) zinaonesha kuwa mwanzo wa milenia hii mahitaji  ya mazao ya wanyama yalikadiriwa kuongezeka zaidi ya mara mbili ifikapo mwaka 2020 ambapo mwelekeo huu wa ulaji wa mazao ya wanyama umeitwa – Mapinduzi katika Ufugaji wa Wanyama.

Matokeo ya utafiti wa kitaifa uliofanyika mwaka 2012/13 pia yalionesha kuwa kaya nyingi zinatemea wanyama kwa ajili ya kujikimu kimaisha na shuguli za maendeleo ya kiuchumi, ambapo wanyama wamekuwa ni vyanzo vya moja kwa moja vya vyakula kama vile nyama, maziwa, na mayai. Pia wanyama kazi ni nyenzo muhimu katika uzalishaji wa mazao wa moja kwa moja katika kilimo kutokana na wanyama hao kutoa mboji inayotumika katika kilimo na uzalishaji wa gesi asilia kwa ajili ya kuzalisha umeme au kupikia na hivyo kuzuia au kupunguza kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega wakati akifungua Mdahalo juu ya vyakula vya asili ya wanyama na mchango wake katika masuala ya afya ya umma na lishe, na uzinduzi wa mikakati ya kitaifa ya kuzuia na kudhibti magonjwa ya brusela na kimeta kwa binadamu na wanyama katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili MUHAS jana jijini Dar es salaam.

Katika ripoti ya Benki ya Dunia inaonesha kuwa nchini Tanzania miongoni mwa kaya zenye mafanikio zaidi huko vijijini na ambazo  zipo katika hatua za kuuaga umaskini, ni zile ambazo zimechanganya shughuli zake na kujumuisha ufugaji.

Ulega ameongeza kuwa Vile vile, Tanzania inashikilia nafasi muhimu ya mafanikio ya kujitosheleza katika mahitaji ya vyakula kwa Bara la Afrika ifikapo mwaka 2050.

Ni wazi kuwa, Kauli Mbiu ya Siku ya Chakula Duniani ya Mwaka Huu “Lishe Bora Kwa Ulimwengu Usio na Njaa” ina maanisha dira ya kuhakikisha kuwa wanyama tuwafugao tunawatumia vyema katika kuchangia kwenye uhakika wa kupata chakula na lishe bora pamoja na usalama wa chakula mbali ya mambo mengine.

Waziri Ulega amesema hivi karibuni Wizara imeanza programu za kudhibiti magonjwa nchi nzima ili kuongeza viwango na ubora wa vyakula vitokanavyo na wanyama.

Miongoni mwa Programu hizo ni Utoaji wa huduma za majosho au dipu kwa ajili ya kudhibiti magonjwa na wadudu kama vile kupe, mbung’o, ndorobo (kwa wanyama), ndigana (kwa binadamu), mbu, homa ya bonde la ufa na wengine watambaao juu ya ngozi za wanyama.

“Mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali ilitumia shilingi milioni 300 kununua dawa za majosho ya wanyama lita 9000 ambazo ziligawiwa kwenye majosho 1,409 nchi nzima na hivyo kutoa huduma hiyo kwa wanyama wengi kama ng’ombe, kondoo na mbuzi”.Amesema Ulega 

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa  tayari mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali imeshanunua lita 11,000 za madawa hayo kwa lengo hilo hilo. ambapo wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa na kupitia miongozo wa Matumizi na Udhibiti wa Madawa ya Majosho ya mwaka 2019 ambayo itaratibu shughuli za majosho ya wanyama hapa nchini na kuifanya kuwa ni wajibu wa lazima kwa kila mfugaji.

Naibu Waziri Abdallah Ulega amesema mwaka wa fedha 2018/2019, jumla ya dozi 301,593,730 za chanjo mbali mbali zenye thamani ya shilingi 17,950,088,000 zilitumika kukinga wanyama dhidi ya magonjwa makuu 11.

Ameongeza kuwa serikali imewekeza juhudi kubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa chanjo na kwa bei nafuu ili Kukiwezesha Chuo Cha Taifa cha Chanjo (TVI) kupanua wigo wa uzalishaji wa chanjo ambapo  kampuni ya Hester Biosciences Limited imealikwa nchini ili kujenga kiwanda cha chanjo hapa Tanzania, na inaandaa ununuzi mkubwa wa chanjo ambazo zitawafikia wafugaji huko vijijini kwa bei nafuu.