Home Mchanganyiko DC CHONJO ATOA SIKU 12 KWA WASIMAMIZI WA MRADI OFISI YA MTHIBITI...

DC CHONJO ATOA SIKU 12 KWA WASIMAMIZI WA MRADI OFISI YA MTHIBITI UBORA WA SHULE MANISPAA YA MOROGORO KUKAMILISHA UJENZI

0

Na Farida Sady, Morogoro

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi.Regina Chonjo ametoa siku 12 kwa wasimmizi wa Mradi wa Ofisi ya Mthibiti ubora wa shule katika manispaa ya  Morogoro kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kukamilisha asilimia nane ya ujenzi iliyobaki sambamba na kutumia kipindi hicho kuweka Samani zote zilizo ainishwa kwenye Mradi.

Kauli ya mkuu wa wilaya inakuja muda mfupi alipotembelea mradi huo na kujione hatua ya ujenzi iliyo fikiwa ,ambapo kwa mujibu wa Mhandishi wa Manispaa Ujenzi umefikia asilimia 92, ingawa muda wa awali uliopangwa kukamilisha ulisha pita.

Aidha mkuu wa wilaya huyo anawataka kusimamia ujenzi na ufanyike usiku na mchana, na katika kipindi hicho cha siku 12 ofisi hiyo ianze kutumika ikiwa na samani zote zinazo hitajika.

Awali kabla ya uamuzi huo Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro  amesema licha ya mradi kuchelewa, mradi umezingatia viwango vilivyo ainishwa kwenye mkataba na dhamira ni kukamilisha sehemu zilizo baki ndani ya kipindi hicho cha nyongeza.

Kukamilika kwa jengo hilo kutarahisisha utendaji katika sekta hiyo muhimu ya elimu, Ikielezwa kuwa kutarahisisha usimamizi na ufuatiliaji jukumu muhimu katika usimamizi wa sekta hiyo.

Jengo hilo la Ofisi ya Mthibiti ubora wa shule hadi kukamilika kwake limepangwa kugharimu kiasi cha shiligi Milion 150, ambapo Manispaa ya Morogoro ni moja katika ya Halmashauri 100 zilizonufaika na mradi huo , unaotekelezwa kwa asilimia 100 na serikali.