Afisa Rasilimali watu wa Kiwanda cha Bia cha TBL Tawi la Mwanza, Dora Nyambalya, akiwakabidhi taulo za kike walimu wa Shule ya Sekondari Mtoni, Rhoda Magesse (kushoto) na Jacqueline Joseph,zilizonunuliwa kutokana na michango ya wafanyakazi.
Walimu wa Sekondari Mtoni Rhoda Magesse na Jacqueline Joseph (katikati) wakifurahi sambamba na Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha TBL tawi la Mwanza,wakati wakipokea taulo za kike zenye thamani ya Shilingi 650,000, zilizotolewa na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Shehena ya vita via hedhi iliyotolewa na wafanyakazi wa TBL Mwanza
…………………..
Katika mwendelezo wa kukabiliana na changamoto ya vifaa vya hedhi kwa wasichana wanaotoka kwenye familia zenye mazingira magumu, wafanyakazi wa TBL wa kiwanda cha Mwanza wametoa msaada wa taulo za kike kwa shule ya sekondari ya Mtoni iliyopo mkoani humo.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya na Arusha nao tayari wameishatoa taulo hizo kupitia taasisi ya Her Africa kwa ajili ya wasichana wanaosoma shule mbalimbali ambao ni walengwa wa msaada huo.
Kwa upande wake Mwalimu, Rhoda Magese, kutoka shule ya sekondari ya Mtoni, iliyopo mjini Mwanza,alishukuru TBL na wafanyakazi wake kwa jitihada za kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii.