JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEFANIKIWA KUZIMA TUKIO LA UJAMBAZI BAADA YA KUKABILIANA NA KUNDI LA WATU WANAOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIHALIFU HUKU WAKIWA WAMEJIHAMI NA BUNDUKI MOJA AINA YA SHOT GUN.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 08.10.2019 MAJIRA YA SAA 8:00 USIKU HUKO KATIKA GODOWN LA CHARLES FAIDA LA VIFAA VYA UJENZI LILILOPO MTAA WA IGOGO TANESCO, WILAYA YA NYAMAGANA KATIKA JIJI LA MWANZA, HII NI BAADA YA KUNDI LA WATU WATANO (5) WANAOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA MOJA AINA YA SHOTGUN YENYE RISASI NNE (4) NA MAPANGA WALIWAVAMIA WALINZI WA KAMPUNI YA ULINZI IITWAYO “JURGON SECURITY GURD” BAADA YA KUWATISHIA KUWAUA KWA SILAHA KISHA KUWAFUNGA KAMBA MIKONONI, MIGUUNI NA BAADAE KUVUNJA GHALA HILO NA KUIBA VITU MBALIMBALI VIKIWEMO PRAISE 60PCS, 2COCK, 100PC, HANGING SCALE 10PC , SPOCK SHAVE 72PC, BOLT NUT PACTS 16, EXPANDED BOLT 12PC.
ASKARI WALIOKUWEPO DORIA WALIBAINI UWEPO WA MAJAMBAZI HAYO KUPITIA KWA WALINZI WA GHALA LA JIRANI NA WALIPOFIKA ENEO HILO JAMBAZI MWENYE SILAHA ALIJARIBU KUWASHAMBULIA ASKARI KWA KUWAFYATUA RISASI NA ASKARI WAKAMKABILI KWA KUMPIGA RISASI JAMBAZI HUYO ALIYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 30-35 AMBAPO ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPELEKWA HOSPITAL HUKU MAJAMBAZI WENGINE WAKIFANIKIWA KUTOROKA.
AIDHA, KATIKA TUKIO HILO JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUKAMATA SILAHA MOJA AINA YA SHOTGUN ILIYOFUTWA NAMBA , IKIWA NA RISASI TATU, GANDA MOJA LA RISASI AINA YA SHOTGUN, MKASI, NONDO, KAMBA ZA KATANI NA MAPANGA MAWILI.
JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA MSAKO MKALI WA KUHAKIKISHA MTANDAO WA MAJAMBAZI HAO UNATIWA NGUVUNI. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA ASKARI YEYOTE ALIYEPOTEZA MAISHA WALA KUJERUHIWA, MALI YOTE ILIYOKUWA IMEIBIWA NA MAJAMBAZI HAO IMEPATIKANA, MWILI WA JAMBAZI HUYO UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA, LINATOA ONYO KWA BAADHI YA WATU WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHALIFU KUWA WAACHE KWANI WATAJIKUTA MARA KADHAA KATIKA WAKATI MGUMU. SAMBAMBA NA HILO TUNAENDELEA KUWAOMBA WANANCHI WATUPE USHIRIKIANO KWA KUTUPA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU MAPEMA ILI TUWEZE KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI.
IMETOLEWA NA,
Muliro J MULIRO-ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
08OCTOBER, 2019