Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akionesha kitabu cha tafiti za mazingira (AFRICA CLIMATE TALKS (ACT3) ), baada ya kukizindua katika mkutano wa wadau wa mazigira kujadili tafiti za wanasayansi zinazohusu mabadiliko ya tabia ya nchi katika ukanda wa bahari. Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akizindua kitabu cha tafiti za mazingira (AFRICA CLIMATE TALKS (ACT3) ), katika mkutano wa wadau wa mazigira kujadili tafiti za wanasayansi zinazohusu mabadiliko ya tabia ya nchi katika ukanda wa bahari.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mazingira katika mkutano wa wadau wa hao kujadili tafiti za wanasayansi zinazohusu mabadiliko ya tabia ya nchi katika ukanda wa bahari.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akizungumza na wadau wa mazingira katika mkutano wa wadau hao kujadili tafiti za wanasayansi zinazohusu mabadiliko ya tabia ya nchi katika ukanda wa bahari.
********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na viwanda zinachangia Kwa kiasi kikubwa kuathiri mazingira hivyo kunatakiwa kuwepo na njia mbadala kuepukana na uchafuzi huo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene katika mkutano wa wadau wa mazigira kujadili tafiti za wanasayansi zinazohusu mabadiliko ya tabia ya nchi katika ukanda wa bahari.
Aidha, Mh.Simbachawene ameongeza kuwa endapo uharibifu wa mazingira utaendelea ikiwemo ukataji miti na uharibifu wa vyanzo vya asili kunaweza sababisha ongezeko la joto kufika nyuzi joto zaidi ya asilimia 2 hivyo bara la Afrika itabidi kuongeza gharama za kupambana na mazingira hadi kufikia dola za kimarekani milioni 530.
“Kama uharibifu wa mazingira ukiendelea waathirika wakubwa ni nchi zinazoendelea na sisi maskini kwani itatuwia vigumu kumudu gharama za kupambana na uharibifu wa mazingira ambao utasababisha uhaba wa huduma za kijamii ikiwemo majanga ya njaa na mafuriko” Amesema Mh.Simbachawene.
Hata hivyo ametoa wito kwa watanzania kulinda mazingira kwa kutokata miti ovyio, uharibifu wa vyanzo vya maji pamoja na kutumia nishati mbadala za kulinda mazingira pamoja na elimu kuendelea kutolewa kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Pamoja na hayo Mh. Simbachawene amezindua kitabu cha tafiti za mazingira (AFRICA CLIMATE TALKS (ACT3) ) ambacho kitawasaidia wao kama serikali kuweka mikakati mizuri ya kisera inayozingatia tafiti zinazofanywa na wataalamu wa mazingira kupambana na uharibifu unaojitokeza kwenye mazingira Duniani.
Kwà upande wake Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mazingira Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Pius Nyanda amesema kuwa kitabu kilichozinduliwa kinaelezea athari za ongezeko la joto baharini ambalo linaathiri upatikanaji wa samaki na wale wanaotegemea uvuvi katika shughuli zao za kila siku.
Prof.Nyanda amesema kuwa kupitia mkutano huo wa siku mbili unaohusisha wataalamu wa ndani na nje ya nchi utawasaidia kuweka mikakati bora na utungaji sera ambazo zitaendana na utunzaji bora wa mazingira katika kuelekea uchumi wa viwanda.