Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiongea na Mama Felista Mkombo baada ya kuamuru ofisi za
Mkjuu wa Wilaya na Mkuu wa Polisi Wilayani Nkasi kumpa shillingi
milioni 15 kama fidia ya kuibiwa ng’ombe zake 25 Mjini Namanyere
wilayani Nkasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisoma mabango kabla ya kuikata utepe kuzindua barabara ya
Sumbawanga-Kanazi mkoani Rukwa leo Oktoba 8, 2019.
Sehemu ya barabara ya Sumbawanga-Kanazi yenye urefu wa kilometa
75 iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli leo Oktoba 8.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akishuhudia wananchi wakijiandikisha katika daftari la mpinga kura
eneo la Nkomolo Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa leo Oktoba 8, 2019.
Akitoa maelezo kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi wilaya ya Nkasi Bw.
Albinus Mugonya.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitunza viaja wa kwaya ya JKT
walipotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Nyamanyere wilaya
ya Nkasi Mkoa wa Rukwa leo Oktoba 8, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia wananchi kijiji cha Chala wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa
akiwa njiani akitokea Sumbawanga leo Oktoba 8, 2019.