Home Biashara NMB yazindua kampeni yake kuwafikishia Watanzania wengi Huduma za kifedha

NMB yazindua kampeni yake kuwafikishia Watanzania wengi Huduma za kifedha

0

Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya dijitali katika kupata huduma za kibenki ijulikanayo  “NMB Mkononi” jna Makao makuu ya benki hiyo.

 ……………………………………………………..
Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi amesema huduma mpya ya dijitali katika kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama NMB Mkononi, iliyotokana na kuunganishwa kwa huduma mbili za NMB Mobile na NMB KLiK, iimeboresha na kuongeza ufanisi kwa watumiaji wa simu za mkononi.

Bw. Mponzi ameyasema hayo katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya wa NMB Mkononi ambayo imeenda sambamba na wiki ya wateja  ulifanyika jana Makao Makuu ya NMB, jijini Dar es Salaam, ambako ilielezwa kuwa huduma hiyo inalenga kuwahakikishia Watanzania wote fursa ya kushughulikia masuala ya kibenki kwa urahisi katika viganja vya mikono yao.

Akisisitiza zaidi kuhusu ubora na tija ya huduma hiyo katika shughuliza kibenki  amesema  benki yake ilikuwa na huduma za
kibenki kwa njia ya simu, lakini imeona umuhimu wa kufanyia kazi mapendekezo ya wateja wao.

Mponzi alifafanua  na kuongeza kuwa maana yake ni Benki Katika Mkono Wako, ambapo mteja anapata huduma zote za kibenki katika mkono wake, kupitia simu yake, wakati
wowote, mahali popote kwa  urahisi na usalama.

“Tunawajali wateja wetu wengi, walioko nchi nzima mijini na vijijini, hivyo tumeona ni vema kuchukua mapendekezo yao ya kubadili NMB Mobile na NMB KLiK kuwa NMB
Mkononi. Najua wapo watakaojiuliza kwa nini NMB Mkononi?

“Kipumbele chetu kikuu ni kuwasaidia Watanzania wote, hata walioko vijijini, kutumia lugha wanayoielewa, tukaona ni vizuri tuje na ‘brand name’ ambayo itawakilishwa kwa Kiswahili na wateja wetu wataona urahisi wa kuijua na kuitumia huduma hiyo,” alisisitiza.

Mponzi alizitaja baadhi ya huduma zinazoweza kupatikana kupitia NMB Mkononi kuwa ni pamoja na kufungua akaunti ya benki hiyo, kutuma na kupokea pesa, kutoa pesa bila kadi ya ATM, kuhamisha pesa kutoka benki moja kwenda nyingine, kulipia bili, tozo na kodi mbalimbali za Serikali.

Aidha, alibainisha kuwa, maboresho hayo ya kihuduma, yataongeza mtazamo chanya wa NMB katika kukuza uwezo na nguvu ya huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo, ikiwa ni shemu ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja chini ya kaulimbiu yao ya – Ubora Uko Hapa!

NMB Mkononi inatarajiwa kufanya mapinduzi  katika kuongeza idadi ya wateja wa  NMB, kutoka Milioni 3.5 wa sasa.

ambapo kwa sasa benki hiyo ina  matawi 230 nchini kote, ikiwa na Mawakala zaidi ya 7000 na mashine za kutolea fedha (ATM) 800.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi wakizindua  huduma mpya ya dijitali katika kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama “NMB Mkononi” katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam jana.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi wakinyoosha bendera ya benki hiyo juu kuashiria uzinduzi wa kampeni ya huduma mpya ya dijitali katika kupata huduma za kibenki ijulikanayo kama “NMB Mkononi” katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam jana.

Kikundi cha ngoma kikitumuiza katika uzinduzi huo.

Waenedsha pikipiki wakionesha michezo mbalimbali kwa kutumia pikipiki kubwa katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wafanyakazi wa NMB waliojishindia zawadi wakionesha zawadi zao.