Jengo la kituo cha umahiri lililopo Musoma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mbele katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Viomgozi wa Serikali, Wizara ya Madini pamoja na Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kushoto, anaefata ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya MadiniIssa Nchasi wakikabidhiwa funguo ya jengo la Umahiri na Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mbele katikati akifanya ukaguzi wa jengo la umahiri kabla ya makabidhiano, mbele kulia ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa, kushoto ni kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara Samwel Mayuki, nyuma kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano, nyuma kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Caroline Mthapula akitoa maelezo juu ya sekta ya madini Mara, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini. Issa Nchasi, anaefata ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na kushoto ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa
Kaimu Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis akiwakirisha taarifa za Kituo cha umahiri cha Musoma
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi akitoa taarifa za kukamilika kwa jengo la kituo cha umahiri Mara
8Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mara
………………..
Na Tito Mselem, Musoma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo leo Oktaba 07, 2019 amekabidhiwa jengo lenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambalo litatumika kama kituo cha umahiri kwa wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Mara.
Jengo hilo lililojengwa na Mkandalasi SUMA JKT na kukabidhiwa kwa Wizara ya Madini kupitia Naibu Waziri Nyongo,nae pia kalikabidhi jengo hilo kwa Tume ya Madini ambapo limekamilika na likotayari kwaajili ya matumizi.
Aidha Jengo hilo la umahiri ni kati ya majengo saba ya umahiri na jengo moja la taaluma lililopo Chuo cha Madini Dodoma (MRI) yaliyojengwa kwa jumla ya thamani ya Bilioni 11.9na SUMA JKT kupitia mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ambayo yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kagera, Musoma, Bariadi, Chunya, Mpanda, Handeni Tanga na Songea.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Naibu Waziri Nyongo ameipongeza SUMA JKT kwa kazi nzuri waliyoifanya ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamika kwa wakati.
Naibu Waziri Nyongo amesema lengo kuu la kuanzisha vituo hivyo ni kuwasadia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za madini kwa tija kwa kuwapatia elimu ya uchimbaji katika vituo hivyo.
“faida ya ujenzi huu ni kutoa mafunzo ya kitaalamu yahusuyo Madini, tutatoa mafunzo ya Utafiti wa Madini, ikiwa ni pamoja na kuonesha mikanda ya Madini ilipo na muelekeo wake, uchimbaji wa madini wenye tija na salama, Uchenjuaji wenye kuleta uvunaji mkubwa wa madini na hivyo kuwapatia faida kubwa wachimbaji”, alisema Nyongo.
Inakadiliwa kuwa baada ya mafunzo kupatiwa kwenye vituo hivi, wachimbaji watavuna madini kwa zaidi ya asilimia 80ukilinganisha na hapo awali ambapo wachimbaji wengi walivuna dhahabu kwa asilimia 30 tu,
Imeelezwa kuwa katika vituo hivi vya umahiri kutakuwa na mafunzo ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kutakuwa na usagaji wa mawe na kupima sampuli mbalimbali za madini.
Aidha Nyongo ametoa rai kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara wakitumie kituo hicho cha umahiri ili viwaletee tija na faidsa katika shughuri za uzalishaji madini.
Kwa upande wake kaimu meneja wa mradi wa usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis alisema kuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ulifanya utafiti wa kijiolojia na kubaini maeneo saba nchini kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya umahiri.
“Utafiti umebaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dhahabu katika eneo la Buhemba yenye takribani wakia 10,737 zenye viwango vya 0.7g/t ndiyo maana kituo hiki kikaja kujengwa hapa Musoma ili kiwasaidie wachimbaji wadogo kupata mafunzo ya namna bora ya uchimbaji madini,” alisema Veronika.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano ameipongeza Wizara ya Madini kwa Kujenga kituo cha umahiri katika Mkoa wa Mara maana kitawasaidia sana wachimbaji kufanya kazi kwa uhakika na sio kubahatisha.