Home Biashara Vodacom Yawapongeza Wateja wake kote nchini

Vodacom Yawapongeza Wateja wake kote nchini

0

Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare (kulia) akimuhudumia Mteja, Peter Mbuya Mkazi wa Tabata Kimanga kwenye duka la Voda lililopo makao makuu ya kampuni hiyo leo, Katikati ni Mtaalam wa Mtandao kutoka Vodacom, Hendrick Rupia. Hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimkabidhi zawadi Emmanuel Machela (34) Mkazi wa Nzuguni Dodoma leo,Kampuni hiyo imekabidhi zawadi hizo  katika wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea. Anayeshuhudia katikati ni msimamizi wa maduka ya Vodacom Kanda ya Kati,Suzana Mwaipopo.

Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimkabidhi zawadi Omari Lubasi mkazi wa Kikuyu Mjini Dodoma leo akiwa ni miongoni mwa wateja waliopata zawadi hiyo katika wiki ya huduma kwa wateja wa Kampuni ya simu ya Vodacom. Anayeshuhudia katikati ni msimamizi wa maduka ya Vodacom Kanda ya Kati, Suzana Mwaipopo na makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi za Vodacom Kanda ya Kati Mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania, Linda Riwa (kulia) akinyanyua juu Champagne kuzinduzi rasmi wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kwenye duka la Voda makao makuu jijini Dar Es Salaam leo. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akimlisha keki mmoja kati ya wateja waliokuwepo dukani siku ya leo.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akizungumza na waandishi na wateja waliohudhuria siku ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, Pia alitoa shukurani kwa wateja na wafanyakazi wa Vodacom kwenye wiki hii na alitoa wito kwa wateja wasajili laini zao kwa alama ya vidole kote nchini.. Kulia ni George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo.