Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) kujadili kuhusu Mradi wa Tanzania Urban Resilience Programme (TURP) unaotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ambao umelenga kuzisaidia Halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika jijini Dodoma.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Maendeleo Mijini na Usimamizi wa Majanga Kanda ya Afrika kutoka Benki ya Dunia Eric Dickson akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuzisaidia Halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi
Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa na Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (kulia) wakiwa katika kikao na Benki ya Dunia (WB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) katika kikao kuhusu mradi wa TURP ambao ukitekelezwa utaleta manufaa makubwa katika Jiji la Dar es Salaam na utaokoa maeneo yaliyo hatari kwa mafuriko na kuyafanya salama kwa maendeleo ya Jiji, utapendezesha kwa kuweka maeneo mazuri ya maegesho ya magari maeneo kwa ajili ya shughuli za umma kama mikutano na matamasha na kubadilisha eneo la Mto Msimbazi linalokumbwa na mafuriko kuwa eneo linalofaa kwa ajili ya michezo na lenye manufaa ya kiikolojia kwa jiji la Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisikiliza maelezo ya mradi kutoka ujumbe wa Benki ya Dunia na Shirika la Mendeleo la Uingereza. kikao kilicofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Raos jijini Dodoma.