Home Michezo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Wambura

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Wambura

0

******************************

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura baada ya kuingia makubaliano na Jamhuri ya kulipa zaidi ya Sh.Mil 100 ambazo alijipatia isivyo halali.
_
Hata hivyo, Wambura atazilipa fedha hizo kwa awamu tano ambapo leo amelipa Mil.20.
_
Wambura alifikishwa Mhakamani hapo kwa mara ya kwanza, Februari 11, mwaka huu , akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh.Mil 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.
_
Wambura ameachiwa huru na Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina.